Monday 25 May 2009

NYUMBANI:TUJIANDAE KATIZO LA UMEME Mei 31


JIJI la Dar es Salaam litaingia kwenye giza nene Mei 31 mwaka huu wakati Shirika la Umeme nchini (Tanesco), litakapozima mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi ya kampuni ya SONGAS.

Taarifa ya Tanesco iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam imesema mitambo hiyo itazimwa kupisha matengenezo ya kawaida katika njia ya kupitishia gesi kwa siku nzima kuanzia saa 10:00 alfajiri hadi saa 12:00 jioni.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kuzimwa kwa mitambo hiyo kutasababisha upungufu wa nishati hiyo kwa megawatti 50 na kusababisha baadhi ya maeneo hayo ya jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.

Maeneo yaliyotajwa kwenye taarifa hiyo kuwa yatakosa umeme ni Wilaya ya Temeke maeneo ya Mwembe Yanga, Tandika Azimio, Tandika sokoni, Kichangani, Temeke Wailes, Temeke Hospital, Maeneo yote ya Yombo, Veternary, Jeje Industry, Petrolube, Tanzania Printers, Metal Product, Kilungule, Tazara flats, Boney M, Vituka, Dovya, Stereo

Wiyani Kinondoni maeneo yatakayoathiri ni Kinondoni Kaskazini maeneo ya M.M.I Steel Industries, Mikocheni B, Kawe Beach, Baadhi ya eneo la viwanda pamoja na kiwanda cha Bidco, Kunduchi Mtongani, Salasala, Baadhi ya maeneno ya barabara ya Africana na viwanda vya Raffia Bag na Family Soap.

Tatizo hilo pia litawakumba wakazi wa Kinondoni Kusini katika maeneo ya Sinza, Manzese, Tandale, Kijitonyama na Mwananyamala.
Taarifa imezidi kueleza kuwa wilayani Ilala umeme hautapatikana katika maeneo ya NSSF Water Front, Tanzania Tea Blenders, Polisi Makao Makuu, TRC, Makao Makuu ya DAWASCO, Keko Mwanga, Mtaa wa Lugoda, Baadhi ya maeneo ya Kariakoo kutokea mtaa wa Msimbazi mpaka Lumumba na Ilala Boma.

Maeneo mengine ni Ilala Sharif Shamba, Ilala Bungoni, Buguruni Malapa, Buguruni Rozana, Buguruni Sokoni, Sehemu ya barabara ya Mandela kuanzia Buguruni mpaka Tabata Dampo, Tabata Liwiti, Tabata Bima, Tabata Mawenzi, Tabata Kimanga na Tabata Kisukuru.

Maeneo hayo ni na Makoka, Kiwalani kwa Gude, Jet Club, Kipawa, Mtaa wa Azikiwe, Mtaa wa Kisutu, Hospitali ya Hindu Mandal, Jengo la Haidery Plaza, Mnazi Mmoja sehemu ya barabara ya Morogoro kuanzia Mtaa wa Kisutu mpaka mtaa wa Samora yatakosa umeme kuanzia saa 10 alfajiri hadi saa 6:00 mchana.

Tanesco imesema umeme utakatika kuanzia saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 jionii katika Mtaa wa Muheza, Mtaa wa Msimbazi, Mtaa wa Nkrumah mpaka Mtaa wa Samora, Upanga Mashariki, Sea View, Kituo cha Polisi cha Salender Bridge, Mitaa ya Uhuru, Magila, Lumumba, Mahiwa na Livingstone.

Imesema pia umeme utakatika sehemu ya barabara ya Bibi Titi kuanzia barabara ya Morogoro, Ally Hassan Mwinyi, DIT, Business College, Hospitali ya Regency, Viwanda vya Zenufa, Mukwano, Bakhresa, Murzah Oil, Vingunguti, sehemu ya Kiwalani, baadhi ya maeneo ya barabara ya Nyerere kuanzia TAZARA mpaka Metrol Steel Kiwalani, Segerea, Kinyerezi na Bunyokwa.

Hali ya umeme itarejea kama kawaida mara baada ya matengenzo hayo kukamilika," imesema taarifa hiyo na kuwaomba radhi wateja

No comments:

Post a Comment

Maoni yako