Saturday 16 May 2009

HUYU NDIYE HAYATI IDD AMIN DADA

Inasemekana kuwa Serikali ya Uganda ina mpango wa kutulipa fidia Watanzania kwa kumwangusha Dikteta Idd Amin kutoka madarakani mwaka 1979 katika vita ile ya Uganda. Hayo yamesemwa na Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki Mhe.Eriya Kategaya,akisema hii itakuwa kama ishara tu ya shukrani kwa namna ambavyo Watanzania chini ya Hayati Mw. J.K. Nyerere walivyojitolea fedha, mali na maisha yao kuhakikisha Nduli Idd Amin anaondoka madarakani na nchi yaa Uganda inakuwa na amani.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako