Monday 13 April 2009

TANESCO YA NYUMBANI


Kwa muda mrefu sasa, bado watanzania wengi tunategemea vifaa hivi kujipatia mwanga wakati wa usiku, huku tukiwa na maparomoko mazuri yenye kuweza kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme. Tuna vito vingi vyenye kuweza kuzalisha umeme, lakini bado rasilimali hizo hazijatumika ipasavyo. Ni vizuri sasa kuangalia namna ya kuendeleza rasilimali hizi ili kumpunguzia mwananchi wa kawaida adha nyingi kutokana na giza la usiku. Msemo mzuri wa Mheshimiwa Rais Kikwete wa kumpatia "Maisha Bora kwa kila Mtanzania" unapaswa kutiwa nguvu zaidi.

Maporomoko mazuri ya Mlima Meru-Arusha

Kituo cha SONGAS-Ubungo
Maporomoko ya Udzungwa Morogoro

No comments:

Post a Comment

Maoni yako