Sunday 23 July 2017

HABARI NJEMA. CCM KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI YATIMA VYUO VIKUU

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wake, Humphrey Polepole kimetangaza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambao wamekosa mikopo ya kuendelea na masomo na wanafunzi ambao ni yatima.

Taarifa iliyotolewa na Polepole inasema kuwa wanafunzi hao wanapswa kufika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kusaidiwa shida zao hizo za mikopo, jambo ambalo limepokewa tofauti na baadhi ya watu wakidai kuwa suala la kutoa mikopo kwa wanafunzi ni jukumu la bodi ya mikopo.

Kutokana na mitazamo ya watu kuwa tofauti katika jambo hili, Humphery Polepole aliibuka na kusema kuwa upinzani wa Tanzania ni mtihani mkubwa kwani wanapojaribu kutatua matatizo ya watu wanakujua juu na wasipotatua matatizo pia wanakuja juu.

"Tukikaa kimya kwa shida za watu inakuwa tatizo, tukishughulika na shida za watu inakuwa tatizo kubwa. Huu upinzani mtihani" alisema Polepole

No comments:

Post a Comment

Maoni yako