Saturday 31 December 2016

TAHADHARI: KWA JOTO HILI .......

Jamani naomba nitoe tahadhari.
Jua limekuwa kali mno na joto kuongezeka sana hasa Dar na kwingineko..viumbe hai vinahangaika makazi hayakaliki...nyoka, nge, tandu ambao si rahisi kuwasikia wanatembea au kutambaa au hata kuwaona wakiwa mbali, wanatafuta maeneo tofauti ya kujihifadhi na hasa kupenya kwenye makazi..nyumba zetu. Mnatahadharishwa kuhakikisha milango na madirisha vimefungwa vema wakati wote kuzuia wasipenye..nyumba zipigwe dawa ndani na nje. jua ni kali na maeneo mengi yana ukame kipindi hiki.

Hii picha ya mamba ni ya leo leo pande za Kigamboni Mwongozo ,amekutwa akizagaa kitaa wananch wakamshughulkia

No comments:

Post a Comment

Maoni yako