Sunday 9 November 2014

MISS TANZANIA 2014 MPYA

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kujiuzuru kwa Sitti Mtemvu aliyekua Miss Tanzania 2014 baada ya kuzuka Sintofahamu kuhusu Umri wake, Lundenga amesema Sitti Mtemvu aliandika barua ya kujivua taji na kuiwasilisha kwa kamati ya Miss Tanzania Novemba 5 2014 ambapo kamati hiyo imeridhia kujiuzulu kwake na kumvua taji.Hivyo taji hili na majukumu ya Miss Tanzania sasa yatachukuliwa na mshindi wa pili Lilian Kamazima aliyekaa kushoto katika picha ambaye taratibu za Miss Tanzania zinamruhusu kuchukua jukumu hilo, Hashim Lundenga ametangaza uamuzi huo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam jana.

Na huyu ndiye anayechukua nafasi ya Redds Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima,aliyekuwa mshindi namba 2

No comments:

Post a Comment

Maoni yako