Sunday 9 November 2014

DILI KWA RAIS MASKINI ZAIDI DUNIANI

Rais wa Uruguay Jose Mujika anasema kuwa amepewa dola millioni 1 ili kuuza gari lake aina ya Volkswagen.
Bwana Mujica ,aliyejulikana kama rais masikini duniani kutokana na maisha yake ,alisema kuwa ombi hilo lilitoka kwa kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu katika eneo la uarabuni.
Aliliambia gazeti la kila wiki la Busqueda kwamba iwapo atalikubali ombi hilo basi fedha hizo zitatumiwa kuwasaidia masikini.
Rais Mujika ambaye anajulikana kama Pepe anaishi katika shamba lake na hutoa pato lake kwa watu masikini.
Mnamo mwaka 2010 Mali yake ilikuwa inagharimu dola 1,800 ambayo ni bei ya gari lake la Volkswagen
Busqueda liliripoti kwamba ombi la gari hilo lilifanywa katika mkutano wa kimataifa mapema mwaka huu katika mji wa Santa Cruz Bolivia.
''Nilishangaa mara ya kwanza ,lakini nikapuuzilia mbali.Ila baadaye ombi jengine lilikuja na hivyo basi nikaanza kulichukulia kuwa swala la umuhimu'',. Alisema Mujika.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako