Thursday 12 December 2013
Waziri Mkuu Mizengo Pinda atoa ya moyoni
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliambia Bunge muda mfupi uliopita kwamba kama ikitokea Rais akamng'oa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu, yeye atafurahi sana kwa kuwa kazi anayoifanya ni mzigo mkubwa.
" Kama ningeambiwa LEO ningeondolewa katika nafasi hii, basi dada Rukia mimi ningefurahi kwa kuwa ningekuwa nimetua mzigo.
"*Dada Rukia, hii kazi huombi, Rais anaangalia na anakuchagua kuwa Waziri Mkuu. Anaweza kuangalia akakuchagua hata wewe dada Rukia, kwa hiyo LEO Rais akisema basi, nianchie ngazi, mimi niko tayari, nitafurahi,*" amesema Pinda katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.
Waziri Pinda ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Rukia aliyetaka kujua msimamo wake kutokana na kauli ya Kamati ambayo yeye na mawaziri wengine waliambiwa wapime kama wanastahili kuendelea kuwa mawaziri kutokana na ufisadi wa kutisha TAMISEMI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako