Bila wasichana warembo kwenye filamu ya kibongo, hakuna atakayeinunua na huenda waandaaji wakaishia kuiangalia tu nyumbani na familia zao
Kwa mujibu wa Tino, wasichana warembo ni ‘chambo’ kinachowavuta wanunuzi wa filamu za Tanzania. Ujuzi wa uigizaji na kipaji, si sababu kwao.
Akiongea na gazeti la Mwanaspoti, Tino alisema warembo hao pamoja na kuzifanya filamu zivutie pia huwa na juhudi katika kazi hiyo tofauti na wanaume na wanaipenda kazi yao.
“Kwa kweli bila kuweka wasichana warembo katika filamu yako hutauza kwa sababu wengi wana juhudi za kufanya mambo mapya kila kukicha, lakini pia wanakuongezea mvuto kwa kuwa warembo ni kama maua,”alisema Tino.
Pengine ndio maana waigizaji wa kike wanaotamba ni walewale akina Wema Sepetu, Lulu, Irene Uwoya, Jacky Wolper, Batulli na wengine waliojaaliwa sura za kuvutia
No comments:
Post a Comment
Maoni yako