Wednesday 11 December 2013
Mrema (MP) kugawana mshahara na wananchu wa jimbo lake kuwainua kimitaji
Wednesday, December 11, 2013Mrema agawana mshahara na wapigakura wake jimboni kwake..!!Mbunge wa Vunjo, Agustine Mrema ( TLP), amesema ameamua kugawana mshahara wake na wananchi wa Vunjo kwa kuwapa mitaji ya biashara kinamama na vijana wa jimbo hilo ili kuendeleza biashara zao na watamrejeshea baada ya nwaka mmoja.
Mrema aliyasema hayo wilayani Moshi wakati akigawa fedha kwenye vikundi vya wajasiriamali na kusema amekuwa akifanya hivyo kila mwaka, lakini wananchi wanamwangusha na kwamba mwaka jana alitoa Sh, milioni 25, lakini zimerudi Sh. milioni tisa tu.
Mrema alisema ameamua kuwa anafanya hivyo baada ya kugundua Watanzania wengi wanakabiliwa na changamoto ya mitaji ya kufanya biashara hasa wajasiriamali wa vijijini.
Vikundi vilivyo nufaika na fedha hizo ni vikundi tisa na kila kikundi kilipata Sh. milioni moja na timu ya mpira ya Kata ya Kahe Mashariki ilipewa fedha kwa ajili ya kuweka magoli ya kisasa katika uwanja uliopo kijiji cha Ghona.
Mwenyekiti wa kikundi cha vijana wa Marangu Mtoni, Harrion Kimati, alisema wanafurahia hatua zinazochukuliwa na Mrema kuhakikisha wanajikimu kwa mitaji.
CHANZO: NIPASHEGumzo
at 3:47 PM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Maoni yako