Thursday 3 December 2015

"VAENI BEJI ZENYE KUONYESHA MAJINA YENU" ASEMA MHE.BALOZI SEFUE

Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao wanapokuwa katika maeneo ya kazi.

Mhe. Balozi Sefue aliutoa mwito huo jana wakati akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza ni kwanini alikuwa amevaa beji yenye jina lake ambayo imemfanya kuonekana tofauti na siku zingine.

Alisema mwishoni mwa mwezi wa kumi na moja alifanya ziara ya kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili na kuagiza watumishi wote wa Umma kuvaa beji zinazowatambulisha majina yao.

“Nimeamua kuonyesha mfano kwa vitendo kufuatia agizo nililolitoa kwa watumishi wa Umma kwa kuvaa beji inayonitambulisha jina langu , nilisema nitakuwa wa kwanza kuvaa jina langu nimevaa. Kama mtumishi wa umma atakuwa na mashaka ajue mimi nimeshalivaa”.

“Mtumishi wa umma anapomuhudumia mwananchi ni lazima ajue amehudumiwa na nani, mtumishi wa Umma akifanya kazi zake kwa kutenda haki sidhani kama ataogopa kuvaa beji inayomtambulisha jina lake hivyo basi kama nilivyoagiza watumishi wote wa Umma mvae beji zinazowatambulisha majina yenu”, alisisitiza Mhe. Balozi Sefue.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako