Saturday, 5 December 2015

DK.KIKWETE AMTAMBULISHA MHE SAMIA SULUHU MAKAMU WA RAIS KWA RAIS WA CHINA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye kitambaa cheupe) akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China (China-Africa Forum) uliofanyika leo Dec 4, 2015 jijini Johannesburg. Mhe. Samia amemwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika mkutano huo
Rais mstaafu wa Awamu ya nne.Dr Jakaya Kikwete jana alijikuta na kazi ya kumtambulisha Makamu wa Rais Mhe Samia Sluu Hasani kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria mkutano wa viongozi wa Afrika na China uliofanyika nchini Afrika Kusini.

Katika sherehe fupi mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo,Dr Kikwete alionekana akizunguka na kuzungumza na vingozi mbalimbali wa Afrika kumtambulisha Mhe Sluu ambaye ameingia madarakani na Mhe Rais Dr Magufuli mwezi uliopita.
Aidha katika tukio lililo vutia hisia za watu wengi haswa baadhi ya maofisa waandamizi wa Serikali ya Tanzania katika mchapalo huo ni kitendo cha Dr Kikwete kumtambulisha Mhe Samia kwa Rais wa China Xi Jinping na kumtaka Rais huyo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania na uongozi mpya chini ya Rais Dr Magufuli

No comments:

Post a Comment

Maoni yako