Monday, 28 December 2015

MAWAZIRI WAPYA 4 NA NAIBU WAAPISHWA


Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Profesa Makame Mbarawa Ikulu, ambapo amewapisha mawaziri watano kujaza nafasi za mawaziri zilizokuwa wazi katika wizara kadhaa za serikali ya awamu ya tano, Hafla ya kuwaapisha mawaziri hao imefanyika leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Gerson Lwenge kuongoza wizara hiyo ikulu leo asubuhi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango kuongoza wizara ya fedha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dk. Joyce Nderichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mawaziri walioapishwa katika picha wa pili kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, wa pili kutoka kulia ni Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kulia ni Mh. George Masaju Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako