Thursday, 24 December 2015

SHOPPInG YA XMAS YAPAMBA MOTO DAR

ZIKIWA zimebaki siku mbili waumini wa dini ya Kikristo duniani kusherehekea sikukuu ya Krismas ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, jana kwa wingi wao, wameonekana wakifanya manunuzi ya nguo na bidhaa mbalimbali za sikukuu katika mitaa ya Kariakoo.
Kamera yetu imefanikiwa kunasa baadhi ya picha zinazoonesha wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wakiwa katika shamrashamra za manunuzi na kusababisha mitaa kutokupitika kwa urahisi kutokana na msongamano wa watu.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako