Monday 3 August 2015

CCM: DKT MAGUFULI KUCHUKUA FOMU YA URAIS NEC KESHO

MGOMBEA mteule wa urais kwa tiketi ya CCM,
Dk. John Magufuli, kesho Jumanne, Agosti 3, 2015, atatinga Tume ya Taifa
ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais katika uchaguzi
mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa
habari, leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye amesema, Msafara wa Dk. Magufuli kwenda kuchukua fomu hiyo,
utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,
Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

Nape amesema, msafara ambao
utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za
Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya
Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshi
la Polisi.

Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombea
mwenza wake, Samia Suluhu Hassan, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM,
atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Dk.Magufuli alichaguliwa na Mkutnao Mku wa CCM, uliofanyika Oktoba 11,
2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose
Migiro na Amina Salum Ally

No comments:

Post a Comment

Maoni yako