Friday 17 January 2014

WACHINA KUTENGENEZA TENA MELI YA TITANIC.

PENGINE TUJIKUMBUSHE KIDOGO KUHUSU MELI YA TITANIC. *Titanic* ilikuwa meli  kutoka Uingereza iliyojengwa kati ya 1909 na 1912 huko Belfast . Wakati ule ilikuwa meli kubwa duniani pamoja na mwenzake "Olympic". Ilipangwa kuzunguka kwenye Atlantiki  kati ya Uingereza na Marekani . Kwenye safari yake ya kwanza iligongana nasiwa barafu  tar. 14 Aprili 1912 mnamo saa sita kasorobo usiku ikazama baada ya masaa 2 na dakika 40 katika usiku wa tar. 15. Aprili 1912. Watu 2200 walikuwepo kwenye meli. Katika maji baridi takriban 1500 walikufa ni 700 waliookolewa na meli zilizokimbia kuokoa watu. Hapa inaonekana "Titanic" ilipotoka bandari ya Belfast  kwa safari za kwanza za majaribio 2 Aprili  1912. Kampuni kutoka China ya Star Investment Group katika mkoa wa Sichuan imesema itatumia dola za kimarekani milioni 165 katika kuijenga upya mpaka kuikamilisha meli hiyo yenye mfano wa Titanic. Katika meli hii ya Replica ni ishara ya uvumbuzi uliopita kikomo kutoka kwa wachina.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako