Saturday 11 January 2014

MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO.

Tunakumbushwa kutimiza wajibu wetu kama wazazi au walezi kwa watoto. Wakati tukijionea matukio mbalimbali ya utovu wa nidhamu,umaskini na uvunjifu wa amani katika jamii,ni dhahiri msemo huo hapo juu wajidhihirisha. Mtoto akilelewa vizuri,hukua vizuri katika nyanja zote za maisha. Lakini asipolelewa vizuri ni chanzo cha vurugu katika jamii. Mtoto huyu anachomeka misumari hii kwenye Yeboyebo ambapo baadae ni hatari kwa wenzake na hata yeye mwenyewe Watoto hawa waonekana kuridhika na walilofanya lakini huku ni.kukosa malezi na tabia hii ikiachwa huzalisha wakorofi, wavutaji bangi,vibaka,majambazi na watu wengine hatari kwa jamii. Kwa upande wa wasichana wasipopata malezi mazuri waweza kufanya hayo nilotaja na hata kujiingiza katika matumizi mabaya ya miili yao kama "machangudoa" tangu wadogo (picha hii ya binti aliyekamatwa akijiuza huko Mwanza ni kwa hisani ya Global Publishers).

No comments:

Post a Comment

Maoni yako