Sunday 19 January 2014

TUMALIZIE WIKI KWA KUPEANA MOYO NA CHANGAMOTO

Japokuwa ni mwanzo tu wa mwaka, kwa wengine tayari maisha yashaanza kuwachosha kiasi cha kukata tamaa. Lakini ni muhimu kuamini kuwa ambalo halijawezekana leo unaweza kujaribu kesho likawezekana. Tusikate tamaa.

Kwa tafsiri ya haraka ni kama vile mtu huyu amekata tamaa. Hiyo ni njia ya treni. Inamaana akiishia usingizini na treni ikipita hapo. Ni kifo tu. Hapo sio sehemu sahihi ya kupumzikia. Bila shaka huyu anataka kufupisha maisha yake kwa kifo hicho. Hapana. Tusikate tamaa. ((SAMAHANI WADAU KWA PICHA HII INAYOFUATA MAANA INAHUZUNISHA SANA.)) Katika picha hiyo ya ajali inayodaiwa kutokea huko Nigeria, dada huyu alipatwa na umauti baada ya kuamua kujilaza relini baada ya ugomvi wa kimapenzi. Jamani hasira hasara. Ni kweli inaumiza kupata na mtafaruko wa kimapenzi lakini isiwe ndo sababu ya kusitisha maisha.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako