Saturday 28 December 2013

MATOKEO YA DARASA LA SABA 2013

WANAFUNZI 16,482 waliofaulu mtihani wa darasa la saba mwaka huu wamekosa nafasi za kujiunga na kidato cha kwanza, kutokana na uhaba wa shule za sekondari nchini. Idadi hiyo ni kati ya wanafunzi 427,609 waliofaulu mtihani huo uliofanyika Septemba 11, katika maeneo mbalimbali nchini, ambapo wanafunzi 411,127 wamechaguliwa kujiunga na sekondari. Matokeo hayo yalitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini, wakati akizungumza na waandishi wa habari.  Sagini alisema wanafunzi waliokosa nafasi wanatoka katika mikoa minane, ikiongozwa na Dar es Salaam yenye wanafunzi 11,796, Mbeya 1,484, Geita 1,578, Dodoma 549, Njombe 379, Morogoro 315, Katavi 261 na Mtwara 120.  Alisema wanafunzi waliokosa nafasi watasubiri hadi Februari mwakani, iwapo watapata shule katika uchaguzi wa awamu ya pili, kutokana na baadhi ya wanafunzi kwenda katika shule binafsi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako