Monday 30 December 2013

MAMBO 10 MUHIMU YA KUWAFANYIA WAZAZI/WALEZI

1. Waonyeshe umekuwa mkubwa
Biashara ya mambo ya kitoto mbele ya wazazi punguza na kama ikiwezekana hata utani wa kijingajinga usio na kichwa wala miguu achana nao. Fikiria kabla ya kuongea na ukumbuke hawa ni matured adults.

*2. Beba Majukumu na Saidia Nyumbani Ukiweza* 
Una mdogo wako anasoma lipa ada, umeshindwa nunua hata madaftari na Uniform tu. Umeona mdogo wako kamaliza shule yupo nyumbani tu mlete mjini alafu msomeshe hata ka kozi ka computer. Baba au mama anajiskia vibaya tuma nauli aje atibiwe Dar na lipa hospital Bills, misaada mingi tu unaweza fanya. Usitegemee kaka au dada zako jitahidi uwe wa kwanza wewe. e.t.c

*3. Muda* 
Tenga muda maalum wa kuwa nao, Imefika Christmass panda basi kakae nyumbani wewe na familia yako. Umepitisha wiki hujawasiliana na mama au baba mpigie simu hata kila weekend. Wafanye wajivunie kuwa wana mtoto anayewajali.

*4. Timiza Ahadi na Usidanganye* 
Hata kama maji yapo vipi shingoni kuwa mkweli kwa wazazi wako. Jitahidi ufunguke mwanzo mwisho. Wamepitia maisha na mambo mengi wanayajua zaidi yako. Umeahidi ntakupigia baadae mama jitahidi upige hiyo simu timiza ahadi. Kuna kitu huwezi fanya wajulishe na sababu utoe sio unaweka ahadi za uongo alafu ukibanwa unazidisha uongo kama mwezi huu hatujalipwa e.t.c

*5. Jitume Kwao* 
Saidia kazi za nyumbani sio unajitia busy na masomo wakati wote. Mama ana mzigo nenda mpokee sio mpaka uitwe. Kama mzazi anasafisha labda chumbani kwake achia unachofanya mshirikiane kwa pamoja. Unajua kupika saidia. Ukiwa na muda osha vyombo nyumbani.

*6. Never Say NO* 
Umetumwa nyanyuka na fanya hapo hapo. Mzazi anavyokwambia kitu ukampotezea ni jambo linaloumiza sana mioyo yao. Huwa wanahisi wamedharaulika na hujihisi wanyonge kwako. Usithubutu kupuuza hata kama wapole vipi kwako. Mara nyingi huwa hawawezi kukwambia kitu ambacho wao wanajua hukiwezi. Hivyo jibu liwe ndio wakati mwingi. Mwanangu nina shida ya hela mjibu ntakutafutia sio sitaki au siwezi.

*7. Wajulishe Hatua Unazopitia Zote* 
Umenunua kiwanja waambie wawemo kwenye furaha yako. Umemuona mchumba unataka KUMUOA mpeleke nyumbani ukamtambulishe. Umepata kazi nzuri waambie na ukihama pia wajulishe. Mke wako kashika ujauzito sema. Baki ya kwamba wazazi wengi wanafurahia sana mafanikio ya watoto wao pia Hili hujenga imani kwao kuwa unawaamini vya kutosha.

***8. Rekebisha Tofauti* 
Umekasirishwa na mzazi ongea nae kwa upole bila kupandisha sauti. Kakuonea ana hasira muache rudi baadae mueleze kinyongo chako. Kununa au kuwaongelea vibaya kwa majirani haifai. Mfano mama amekuudhi sana na una feel comfortable kwa baba basi mueleze baba linalokukera.

***9. Zawadi* 
Mama hana kanga nzuri jitoe kimasomao ndo ukubwa. Nunua hata ndala tu za mzazi kama zinaonyesha dalili ya kuisha. Zawadi ndogo ndogo ni silaha kubwa sana kwa wazazi maana huonyesha unawajali toka ukiwa na umri mdogo. Umeenda likizo nyumbani na watoto hakikisha unabeba chochote. Ukitaka kujua wazazi wanathamini sana zawadi ni wakati unarudi kwako lazima utafungashiwa tu chochote kile kwenye kiroba hata machungwa tu.

*10. Sifa* 
Mmekaa wawili na mzazi toa shukrani kwake kwa kila jema alilokutendea. Msifu kwa wema wake na umwambie kwanini unajihisi una bahati kumpata yeye kama mzazi. Kumbuka wazazi wamefanya mengi sana kwako kuliko hata unayoyajua. Usichoke kushukuru na kuwamwagia sifa. Wafanye watambue kuwa wao ni mfano mzuri sana wa kuigwa na hawajakosea hata kitu kimoja katika malezi yako. Shukrani zikiambatana na vitendo kama Kumkumbatia mama au baba wakati zinatolewa huwa zinapendeza zaidi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako