Tuesday 10 December 2013

Kumbe Mandela aliwahi kuishi na familia ya Kichagga ya Swai

Katika mwaka wa 1962 Nelson Mandela aliondoka Afrika kusini kisirisiri na kwa muda wa miezi saba alikuwa akitembelea mataifa mengi ya bara la Afrika. Chama cha African National Congress, ambacho kilikuwa ndio kimepigwa marufuku na utawala wa ubaguzi, kilikuwa kimeanzisha mapambano ya kijeshi kupitia jeshi lake la Umkhonto we Sizwe. Kazi ya mandela ilikuwa ni kutafuta uungwaji mkono wa hali na mali kutoka mataifa mengine ya Afrika na pia kutafuta mataifa yaliyo tayari kuwapa mafunzo ya kijeshi makurutu wake akiwemo yeye mwenyewe. Alipata mafunzo ya kijeshi nchini Morocco, kutoka kwa wanajeshi wa Algeria waliokuwa wanatumia ardhi ya Morocco kama kituo chao kupigana dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ufaransa.Mafunzo mengine yalifanyika Ethiopia. Katika kuangalia safari ya maisha ya Nelson Mandela zipo taarifa kwamba kabla ya kufungwa jela, Marehemu Nelson Mandela aliwahi kuishi nchini Tanzania katika familia moja ambapo wakati anaondoka aliacha baadhi ya vitu vyake vikiwepo viatu
Mandela na mkewe Winnie akiwa ameshika viatu vyake alivyorudishiwa toka familia ya Swai alipotembelea Tanzania mwaka 1997 Viatu vya Mandela alivyoacha Tanzania na baadae kukabidhiwa tena salama

No comments:

Post a Comment

Maoni yako