Saturday 13 June 2009

CRISTIAN RONALDO KUHAMIA SPAIN


Hatimaye timu ya soka ya Uingereza ya Manchester United imeafiki kitita cha fedha kilichovunja rekodi ya mauzo ya mchezaji duniani cha paundi milioni 80 kwa Criostiano Ronaldo ajiunge na Real Madrid.

Taarifa kutoka klabu ya Old Trafford imesema "United imeafiki kuiruhusu Real Madrid kufanya mazungumzo na mchezaji".

Taarifa hiyo imeongeza kueleza kwamba uamuzi huo umekuja kutokana na maombi ya Ronaldo mwenyewe baada ya "kwa mara nyingine kuonesha hamu ya kuondoka".

United imelezea zabuni hiyo kwa mshabuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kama isiyokuwa na masharti na kuongeza wanatumaini makubaliano kamili yatafikiwa mwishoni mwa tarehe 30 mwezi huu wa Juni.

Imefahamika kwamba fedha za uhamisho zitapatikana kwa meneja wa Mashetani hao Wekundu Sir Alex Ferguson kwa ajili ya kuwekeza katika soko la usajili.

Madrid tayari mapema wiki hii ilimsajili kiungo mshambuliaji Mbrazil kwa kitita inachosemekana ni paundi milioni 56 na kukipiga kumbo kiasi kilichokuwa juu cha fedha kumsajili mcghezaji duniani, kilichokuwa kikishikiliwa cha paundi milioni 45.6 ambacho Real ililipa kumpata Zinedine Zidane 2001.

Madrid pia inaelezwa kuwa na uchu kuwachukua Xabi Alonso wa Liverpool, David Villa wa Valencia na winga wa Bayern Munich Franck Ribery.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako