Wednesday 17 June 2009

BEI ZA MAFUTA JUU TENA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) Haruna Masebu akifafanua jambo juu ya mwenendo wa bei za mafuta hapa nchini kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali jana katika ofisi za mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) Haruna Masebo amesema kuwa kutokana na biashara ya mafuta hapa nchini ni huria mamlaka imepewa jukumu la kufuatilia mwenendo wa biashra hiyo kwa karibu zaidi lengo kuu ni kujiridhisha kuwa nchi inakuwa na akiba ya ziada ya mafuta. Mafuta kwa sasa hivi yameanza kupanda bei kwa baadhi ya vituo. Azma ya EWURA ni kuhakikisha mafuta yanauzwa kwa bei ya kawaida kulingana na soko na kwa kutumia miundo mbinu salama hii inatokana na unyeti wa bidhaa za mafuta na umuhimu wake katika maendeleo.

Masebo alisema mwenendo wa bei za mafuta hapa nchini na katika soko la Dunia kwa kipindi cha mwezi Januari hadi juni 2009 bei za mafuta ya aina ya zote nchini zimekuwa za zikipanda japo si kwa kasi kubwa kama ilivyokuwa kwa mwaka jana. Kupanda kwa bei za mafuta kumetokana na sababu kuu mbili ambazo aalizitaja. Moja ni ongezeko la bei kununulia mafuta kwenye soko la dunia kwa Petroli bei imepanda asilimia 46.31,dizeli asilimia 11.98 na mafuta ya taa asilimia 6.42 katika kipindi cha kati ya mwezi Januari na mwishoni mwa mwezi Mei 2009. Mfumuko (inflation) wa bei hapa nchini ni asilimia 13.3.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako