Saturday, 19 September 2009

SAFARINI

Kumradhi wadau, nilipata safari ya ghafla kuelekea Kijijini kwa Bibi na Babu kuhani msiba wa Baba yangu mzazi, na mtandao huku hakuna kabisa. Muda mfupi ujao nitarudi na kuwaletea yaliyojiri.
Salaam kutoka Kijijini

Tuesday, 1 September 2009

KOMOA UKOMOLEWE ! au BILA BILA!

KARIBU DAR ES SALAAM ZOO

Watanzania wenzangu,kumbe kuna fahari yetu imejisimika ndani ya DAR ES SALAAM ZOO, tujongee tukajionee wenyewe kama kwenda Serengeti au Ngorongoro ni Mbali, basi hapa patakidhi haja yako.
Taarifa hizi ni kwa hisani ya:
www.daressalaamzoo.com na Michuzi

Monday, 31 August 2009

MASANJA WA ORIJINO KOMEDI KWENYE BLOG

Masanja nae kaibuka kwenye blog na amekuja na kitu kinaenda kwa jina la
www.mkandamizaji.blogspot.com
Karibuni wadau kwenye kiwanja kipya hicho.

MWISHO WA MWEZI

Mwisho wa mwezi umewadia, tunapoganga yaliyopita,pengine picha hii inaweza kukukumbusha mengi. Zingatia kusamehe waliochukizwa na mafanikio yako, na jitahidi kuimarisha mafanikio uliyopata mwezi mzima,na yawe kichocheo cha mwezi ujao. Jitahidi kupunguza wakuchukiao kwa kuwa "mtu wa watu", na pengine kwa kuweka mipaka.
Nawatakieni nyote Mwisho mwema wa mwezi na mwanzo mwema wa wiki.

Sunday, 30 August 2009

WADAU NAWATAKIENI JUMAPILI NJEMA

"Bila msaada wa Bwana ,kazi zenu ni bure....." Tujitahidi kumweka Mungu mbele katika yote nae atatujalia yale tuyahitajio. Ni siku nyingine ya kumsifu yeye kwa namna ya pekee, tuitumie vema. Pia ni wakati wa mapumziko kwa wengine, basi mapumziko mema.

Punda afe,mzigo ufike!!

Saturday, 29 August 2009

NOTI MPYA YA SHILINGI 2,000



BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa noti mpya za Sh2,000 ambazo zitatumika sanjari na zilizopo kwenye mzunguko kwa sasa.

Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba, lengo la kutoa noti hizo mpya ni kukidhi mahitaji yake kwenye mzunguko wa fedha nchini.
"Noti hizi mpya zinatofauti moja tu na zile ambazo zimo kwenye mzunguko kwa sasa nayo ni saini zilizopo.

Saini zilizopo kwenye noti mpya ni za Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania,” alisema.
Profesa Ndulu alisema kuwa noti hizo bado zina rangi ya kahawia, zikiwa na michoro inayoonyesha mandhari ya kitanzania kiuchumi, kiutamaduni pamoja na urithi wetu na mazingira.

"Mbele ya noti, bado kuna picha inayoonyesha utajiri wetu wa kuwa na mojawapo ya wanyama pori wakubwa yaani simba ,alama ya kificho ya twiga ambayo bado ipo kama ilivyo katika noti nyingine zinazozunguka sasa" lilifafanua tangazo hilo.
Alama nyingine zilizopo katika noti hiyo ambazo hazina tofauti na iliyopo kwenye mzunguko ni nyuma ya noti kuna picha inayoonyesha picha ya ngome kongwe illiyopo Forodhani jijini Zanzibar.

Vile vile, alisema zina picha ya kinyago cha kuchonga na alama ya usalama inayobadilika rangi ikigeuzwa.
”Benki kuu inawashauri wananchi kuwa hakuna haja ya kubadili noti hizo kwani thamani yake ni ileile na kwamba haina mpango wa kuzifuta zilizokuwepo katika mzunguko wa awali.

Habari imeandikwa na Burhani Yakub wa gazeti la Mwananchi.

ASILI YETU ZAMANI HIZO

LOH, KUMBE NA SISI TUNA VIFAA!!

Hivi na vingine vingi vilionyeshwa siku ya Maadhimisho ya Miaka 45 ya JWTZ