Tunapokuwa katika harakati za kuboresha maisha na kuinua kipato, tukijaaliwa na mola tukumbuke katika matumizi yetu na matendo yetu ya kila siku kuwa kuna watoto wengine wanatafuta elimu kwa kusomea chemli, kuna wanaoenda shuleni nguo zimechania na hawana njia mbadala ya kujikwamua.
Thursday, 6 December 2012
Wednesday, 5 December 2012
WIZI MTUPU
Picha hii inanikumbusha ule ujanja wa mbuni kuchimbia kichwa chacke kwenye kichaka huku mwili wote upo nje kana kwamba anajificha. Huyu jamaa ni vyema akaenda kijijini kulima matembele kulikoni kuendelea na usanii huo maana siku wajanja kama mie tukimgundua, ni kichapo cha mbwa mwizi. Kipofu anasoma message,anaandika title tena kwa kiingereza, wapi na wapi?
Tuesday, 4 December 2012
VIPAJI TULIVYONAVYO BINADAMU
Hii ni live, dada Angel alipotembelea Mbuga za wanyama Afrika ya Kusini. Hapa ni sehemu wanapoita "Lion Encounter"
UTAFUTAJI WA KIMASHA MASHAKA
Hii inanikumbusha msemo "Punda afe mzigo ufike", Ni kweli tunapaswa kujitahidi kutafuta, lakini ni kwa namna gani tunatafuta na tunanufaika vipi na utafutaji huo. Mwisho wa siku upakiaji huu wa bidhaa hii kwenye hili gari wahatarisha maisha na uharibifu zaidi kuliko faida ipatikanayo.
UJUMBE WA LEO
Ndege anapokuwa hai huwa anakula sana funza, lakini atakapokufa funza humla yeye.
Maisha hubadilika kila wakati hivyo usimdharau wala kumuumiza mtu yeyote katika maisha.
Unaweza kuwa imara saaana leo lakini kumbuka maisha ni imara kuliko wewe.
Mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima.
Kuwa mwema kwa kila mtu.
Maisha hubadilika kila wakati hivyo usimdharau wala kumuumiza mtu yeyote katika maisha.
Unaweza kuwa imara saaana leo lakini kumbuka maisha ni imara kuliko wewe.
Mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima.
Kuwa mwema kwa kila mtu.
Monday, 3 December 2012
WIKI IMEANZA
Pilika pilika za maisha zimeanza tena. Ni mwanzo wa wiki, nami nawatakia wadua kila la kheri katika uchacharikaji wa kufanya maisha kuwa bora zaidi.
Sunday, 2 December 2012
SIDHANI KAMA INASAIDIA
Jana tulikuwa tunaadhimisha siku ya Ukimwi Duniani, nikamwona huyu jamaa yangu na kujiuliza kama hii ndo gear ya kuzuia maambukizi, basi hapa atakuwa mbali na ukweli au unasemaje mdau. Samahani kwa picha hii kama itakukwaza lakini ni kufikisha ujumbe tu.
ASUBUHI NJEMA
Mwaka unapokaribia ukingoni tunalazimika kutathmini mafanikio na vikwazo vya maendelea. Lakini kwakuwa bado tuna mwezi mmoja si vibaya kujitahidi pale ambapo bado juhudi haijawa ya kutosha.
Subscribe to:
Posts (Atom)