Friday 7 March 2014

MWANAMKE MWENYE UMRI MKUBWA KWA SASA DUNIANI

Misao Okawa, ambaye aliwekwa kwenye kitabu cha rekodi kubwa za dunia ‘Guinness’ mwaka jana kama mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani, juzi (March 5) amefanya sherehe ya siku ya kuzaliwa baada ya kufikisha umri wa mika 116.
Misao ambaye anaishi chini ya uangalizi na matunzo huko Osaka, Japan alitangazwa rasmi kuwa mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani baada ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo kufariki.
Ingawa umri wake ni mkubwa sana, anaonekana bado ana afya nzuri na aliweza kuipuliza mishumaa yake kama mtu mwingine.

Hata hivyo yawezekana kuna watu wenye umri mkubwa zaidi yake sehemu fulani duniani ila kwakuwa hawajaweza kufikiwa na vyombo vya habari imekuwa ngumu kuwatambua. Mungu ana yake mengi hatuwezi jua yote.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako