TUJIFUNZE KUMUHESHIMU KILA MTU HATA KAMA UNA MALI NYINGI KIASI GANI IPO SIKU NA WEWE UTAKOSA -
Wadau tukumbuke hali ya maisha huweza kubadilika wakati wowote.
Leo waweza kuwa tajiri lakini kesho ukawa masikini.Endapo unaamini hayo yanaweza tokea wakati wowote, basi huna budi kumuheshimu yule asiye nacho,au aliye na kidogo kuliko wewe kwasababu wakati wowote unaweza ukawa katika hali aliyonayo mwenzako
(Picha maeneo fulani Kariakoo Dar)
Wednesday, 28 January 2015
MJUE MWANASHERIA MKUU MPYA WA SERIKALI
Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali ya Tanzania mhe.George Masaju akila kiapo katika ukumbi wa Bunge hii leo baada ya Jaji Werema kujiuzulu
Spika wa Bunge mhe. Anna Makinda aiingia katika Ukumbi wa Bunge Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine alimwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Spika wa Bunge mhe. Anna Makinda aiingia katika Ukumbi wa Bunge Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine alimwapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Tuesday, 27 January 2015
ZAMBIA YAPATA RAISI MPYA
Rais mpya wa Zambia Mhe. Edgar Lungu akila kiapo kushika hatamu baada ya bnafasi ya urais kuachwa wazi kufuatia kifo cha Rais Sata.
Sunday, 25 January 2015
MABADILIKO: UTEUZI WA MAWAZIRI NA MANAIBU
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amebadili mawazini na naibu mawaziri Ikulu jana.
Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao jana, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais, Sifue Ombeni alitaja mawaziri hao wapya ambao wanaapishwa jana jioni hii na wizara zao kwenye mabano kuwa George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).
Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).
Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini).

Saturday, 24 January 2015
Friday, 23 January 2015
ELIMU HAINA MWISHO
Bibi huyu mkazi wa Kenya kaamua kurudi shule ili kujifunza kusoma na kuandika. Hakuna kuchelewa katika kujifunza jambo jipya
Thursday, 1 January 2015
KHERI YA MWAKA MPYA 2015
Napenda kuungaana na wadau wapendwa wa blog hii kumshukuru kwa kutuwezesha kuuona Mwaka Mpya 2015. Tunazidi kumwomba Mungu atuongoze kwa mwaka huu wote ili tuweze kutimiza majukumu na matarajio yetu kwa baraka zake.
Subscribe to:
Posts (Atom)

.jpg)