Wednesday, 8 January 2014
Tuesday, 7 January 2014
SHUKURU ULIVYOUMBWA
Huyu ni mwanadada ambaye sehemu kubwa ya maumbile yake yanaonekana ya kiume.
Mwanaume huyu kutoka Indonesia anasumbuliwa na vipele hivi tangu miaka ya 90 baada ya kufanyiwa upasuaji fulani kiunoni.
Monday, 6 January 2014
JEURI YA FEDHA
Jumba la kifahari la mwanamuziki Rihanna huko Los Angeles.
Gari la kifahari aina ya Range Rover iliyopambwa nakshi na sarafu za dhahabu huko Uarabuni
Kampuni ya magari ya Marcedes Benz yatoa gari inayojiendesha yenyewe.
Meli kubwa na ya kifahari yenye huduma za kila namna ndani
PILIKA ZIMEANZA
Juma jipya la kwanza la mwaka huu lililo kamili limeanza. Kila mmoja yupo ktk kutafuta kipato kwa njia halali. Nawatakia wadau wote na watafutaji halali kila jema ktk kuboresha maisha kwa mwaka huu.
Ila kwa wale waliopewa dhamana mbalimbali katika jamii,ni muhimu katika kuwajibika kwao waangalie adha hii wanayopata baadhi ya wananchi ktk maisha yao ya kila siku.
"something should be done because this is not fair"
Sunday, 5 January 2014
Saturday, 4 January 2014
USAFIRI WA DALADALA DAR WAZIDI KUWA KERO.
Abiria wakisubiri usafiri kuingia jijini katika kituo cha Mbezi Mwisho leo asubuhi.
Kila kukicha kero za usafiri wa Daladala jijini dar wazidi. Kwa nyakati za asubuhi vituo vya Mbagala, Mbezi Mwisho,Kimara mwisho,Gongola mboto na vinginevyo no shida tupu. Jioni Posta,kivukoni,Fire ,Bahkresa ,Akiba na Msimbazi ni patashika.
Friday, 3 January 2014
BENKI KUU TANZANIA YATOA SARAFU YA 50,000
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa sarafu maalumu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye thamani ya sh 50,000. Sarafu hiyo haitaingizwa kwenye mzunguko wa fedha wala kutumika kwa malipp yoyote.
Habari zaidi angalia www.dj sek.blogspot.com
KILA JAMBO KWA KIPIMO
Ni mwanzo tu wa mwaka 2014. Itakuwa jambo zuri kujipima kiutendaji na pale unapoona pana upungufu ni busara kutafuta mbinu za kufanikiwa zaidi binafsi na hata ikibidi kuomba ushauri.
Si busara sana kung'ang'ania jambo ambalo yaonekana huwezi kwa kipimo cha uwezo wako mwenyewe. Kuna mwenzio anaweza zaidi,mpe nafasi ya kukusaidia aidha mbinu au hata kutekeleza kwa ushirikiano. Ubinafsi sio tija mwaka 2014.
Thursday, 2 January 2014
LIONEL MESSI AKWEA MLIMA K'NJARO
Wakati mchezaji mashuhuri wa dunia wa club ya Barcelona amekwea mlima Kilimanjaro kwa hisani ya Turkish Airlines,nasi watanzania tujiulize mlima huo kama kivutio cha utalii na raslinali ya taifa, je wawaza nawe siku.moja kukwea au unadhani ni.watu kutoka nje ya nchi tu?
Wednesday, 1 January 2014
HAPPY NEW YEAR 2014
Naungana na watu wote duniani kuukaribisha mwaka mpya 2014. Nawatakia Heri ya Mwaka Mpya wadau wangu wote. Nawaombea na kuwahimiza uwe mwaka wa amani. Tuchape kazi kwa bidii. Tuwe wenye kueneza furaha na upendo kwa wote. Hata kama katika kuwajibika tutajikuta bado hatujafikia malengo tusikate tamaa. " FORWARD EVER. BACKWARD NEVER"
Subscribe to:
Posts (Atom)