Thursday, 12 December 2013

Waziri Mkuu Mizengo Pinda atoa ya moyoni

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameliambia Bunge muda mfupi uliopita  kwamba kama ikitokea Rais akamng'oa katika nafasi yake ya uwaziri mkuu, yeye  atafurahi sana  kwa kuwa kazi anayoifanya ni mzigo mkubwa. " Kama ningeambiwa LEO ningeondolewa katika nafasi hii, basi dada Rukia mimi ningefurahi kwa kuwa ningekuwa nimetua mzigo. "*Dada Rukia, hii kazi huombi, Rais anaangalia na anakuchagua kuwa Waziri Mkuu. Anaweza kuangalia akakuchagua hata  wewe dada Rukia, kwa hiyo LEO Rais  akisema basi, nianchie ngazi, mimi niko tayari, nitafurahi,*" amesema Pinda katika kipindi cha maswali na majibu bungeni. Waziri Pinda ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Rukia aliyetaka  kujua  msimamo wake kutokana na kauli ya Kamati ambayo yeye na mawaziri wengine waliambiwa wapime kama wanastahili kuendelea kuwa mawaziri  kutokana na ufisadi wa kutisha  TAMISEMI.

Wednesday, 11 December 2013

Uzalendo wa Mandela

Kazaliwa nchini kwake, Kakulia nchini kwake, kaugulia nchini kwake, Kalazwa nchini kwake, Katibiwa nchini kwake, Kafia nchini kwake, Atazikwa nchini kwake.

Mrema (MP) kugawana mshahara na wananchu wa jimbo lake kuwainua kimitaji

Wednesday, December 11, 2013Mrema agawana mshahara na wapigakura wake jimboni kwake..!!Mbunge wa Vunjo, Agustine Mrema ( TLP), amesema  ameamua kugawana mshahara wake na wananchi wa Vunjo kwa kuwapa mitaji ya biashara  kinamama na vijana wa jimbo hilo ili kuendeleza biashara zao na watamrejeshea baada ya nwaka mmoja. Mrema aliyasema hayo wilayani Moshi wakati akigawa fedha kwenye vikundi vya wajasiriamali na kusema amekuwa akifanya hivyo kila  mwaka, lakini wananchi wanamwangusha na kwamba mwaka jana  alitoa Sh, milioni 25, lakini zimerudi Sh. milioni tisa tu.  Mrema alisema ameamua kuwa anafanya hivyo baada ya kugundua Watanzania wengi wanakabiliwa na changamoto ya mitaji ya kufanya biashara hasa wajasiriamali wa vijijini.  Vikundi vilivyo nufaika na fedha hizo ni vikundi tisa na kila kikundi kilipata Sh. milioni moja na timu ya mpira ya Kata ya Kahe Mashariki ilipewa fedha kwa ajili ya kuweka magoli ya kisasa katika uwanja uliopo kijiji cha Ghona.  Mwenyekiti wa kikundi cha vijana wa Marangu Mtoni, Harrion Kimati, alisema wanafurahia hatua zinazochukuliwa na Mrema kuhakikisha wanajikimu kwa mitaji.  CHANZO: NIPASHEGumzo  at 3:47 PM

Taifa Stars yatolewa Chalenji

TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' imeondolewa kwenye michuano ya Kombe la Chalenji inayoendelea nchini Kenya baada ya kufungwa na timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' bao1-0 katika mechi iliyomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Nyayo uliopo jijini Nairobi

Tuesday, 10 December 2013

Kumbe Mandela aliwahi kuishi na familia ya Kichagga ya Swai

Katika mwaka wa 1962 Nelson Mandela aliondoka Afrika kusini kisirisiri na kwa muda wa miezi saba alikuwa akitembelea mataifa mengi ya bara la Afrika. Chama cha African National Congress, ambacho kilikuwa ndio kimepigwa marufuku na utawala wa ubaguzi, kilikuwa kimeanzisha mapambano ya kijeshi kupitia jeshi lake la Umkhonto we Sizwe. Kazi ya mandela ilikuwa ni kutafuta uungwaji mkono wa hali na mali kutoka mataifa mengine ya Afrika na pia kutafuta mataifa yaliyo tayari kuwapa mafunzo ya kijeshi makurutu wake akiwemo yeye mwenyewe. Alipata mafunzo ya kijeshi nchini Morocco, kutoka kwa wanajeshi wa Algeria waliokuwa wanatumia ardhi ya Morocco kama kituo chao kupigana dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ufaransa.Mafunzo mengine yalifanyika Ethiopia. Katika kuangalia safari ya maisha ya Nelson Mandela zipo taarifa kwamba kabla ya kufungwa jela, Marehemu Nelson Mandela aliwahi kuishi nchini Tanzania katika familia moja ambapo wakati anaondoka aliacha baadhi ya vitu vyake vikiwepo viatu
Mandela na mkewe Winnie akiwa ameshika viatu vyake alivyorudishiwa toka familia ya Swai alipotembelea Tanzania mwaka 1997 Viatu vya Mandela alivyoacha Tanzania na baadae kukabidhiwa tena salama

Monday, 9 December 2013

UZALENDO:Taifa Stars yaingia nusu fainali Chalenji

*TIMU ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kusonga mbele hatua ya Nusu Fainali baada ya kuwatoa Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Uganda kwa ushindi wa changamoto ya penalti 3-2 katika michuano ya kombe la Chalenji inayoendelea jijini Nairobi, nchini Kenya lakini shujaa akiwa kipa Ivo Mapunda .**Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Manispaa ya mji wa Mombasa nchini Kenya, Uganda ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza likifungwa na Daniel Sserunkuma katika dakika ya 16 akimalizia krosi ya Khamis Kiiza, bao ambalo halikudumu sana kabla ya Mrisho Ngassa kuisawazishia Stars kwa shuti kali 18.* *Baada ya bao hilo Stars walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la pili likifungwa na Ngassa kwa mpira wa adhabu uliojaa wavuni katika dakika ya 39, matokeo ambayo yalidumu mpaka mwisho wa kipindi hicho cha kwanza.**Kipindi cha pili Stars inayofundishwa na kocha Kim Poulsen, raia wa Denmark, ilipata pigo katikati ya kipindi hicho baada ya kiungo wake Salum Abubakar 'Sure Boy' kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu, ambapo nafasi hiyo iliwapa nguvu Uganda kupata bao la kusawazisha kupitia Martin Mpuga matokeo ambayo yalibaki hivyo mpaka mwisho wa mchezo na kuzipeleka mpaka kwenye matuta. Katika mikwaju ya penalti Ivo alikuwa shujaa baada ya kucheza penalti mbili za Waganda ya beki  Khalis Alucho na  ile ya mwisho iliyopigwa na Sserunkuma ambayo ndiyo iliyoivusha stars. *

Mandela kupewa mazishi ya kihistoria

*MAZISHI ya Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela, yanatarajia kuweka rekodi ya dunia kwa kuhudhuriwa karibu na marais 140 kutoka sehemu mbalimbali duniani. Taarifa iliyochapishwa na Gazeti la DailyMail la Uingereza jana, ilisema viongozi hao wataungana na familia na wananchi wa Afrika Kusini. ** Lakini kwa mujibu wa gazeti hilo, Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, hatohudhuria mazishi ya Mandela baada ya kushauriwa na jopo la wasaidizi wake. Jopo hilo lilisema kutokana na umri mkubwa alionao Malkia Elizabeth hataweza kuhimili mwendo mrefu wa ndege kutoka Uingereza hadi Afrika Kusini. Kutokana na hali hiyo, Malkia Elizabeth atahudhuria misa maalumu iliyoandaliwa katika Kanisa la Westminster Abbey mjini London na kusaini kitabu cha kumbukumbu.  Gazeti hilo lilisema tayari Rais wa Marekani, Barack Obama na marais wastaafu wa nchi hiyo, George W. Bush na Bill Clinton na wake zao, Hillary Clinton na Laura Bush wataungana na viongozi wengine watakaoaga mwili wa Mandela katika Uwanja wa Taifa wa Afrika Kusini wa First National Bank (FNB).  Taarifa ya Ikulu ya Marekani ilisema marais hao wote watatumia ndege moja ya Airforce One.  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais mstaafu, Bush atahudhuria mazishi ya Mandela baada ya kukubali mwaliko aliopewa na Rais Obama. Viongozi wengine ambao wamethibitisha kuhudhuria mazishi hayo ni Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, Kiongozi wa Kidini wa Jimbo la Tibet, Dalai Lama, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ambaye jana alitarajia kuondoka nchini Ufaransa kuelekea Afrika Kusini.** **Misa **Askofu mstaafu, Desmond Tutu, anatarajiwa kuongoza misa ya mazishi.  Habari zinasema zaidi ya watu 80,000 wanatarajiwa kuuaga mwili wa Nelson Mandela katika Uwanja wa FNB uliopo mjini Soweto, Johannesburg.  Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa familia ya Mandela, Temba Matanzima, alisema Serikali imeandaa utaratibu ambao utaelekezwa kwa maelfu ya wananchi watakaohudhuria uwanjani hapo kutoa heshima za mwisho.  Jana asubuhi, maelfu ya wananchi wa Afrika Kusini walikusanyika katika makanisa, misikiti, masinagogi na maeneo mbalimbali kwa ajili ya kumuombea Mandela ambaye alifanikiwa kuleta mapatano katika Taifa hilo bila kujali rangi, makabila wala tofauti za kidini.  Shughuli za kumuombea Mandela zimedumu kwa siku kadhaa tangu Desemba 6, mwaka huu, baada ya Rais Jacob Zuma kutangaza kifo cha shujaa huyo. Wananchi wa Afrika Kusini wataanza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Mandela kesho na kesho kutwa yaani Desemba 11 mwili wa kiongozi huyo utapelekwa Ikulu ya Pretoria. Desemba 14, mwili huo utasafirishwa kwa ndege ya kijeshi hadi mji wa Mthatha, ambako utabebwa kwa gari maalumu kuelekea katika Kijiji cha Qunu na siku inayofuata atazikwa. Rais Zuma alisema: “Shughuli ya kuagwa Mandela itafanyika kwa uwazi na tutazingatia vigezo vyote vya urithi wake. Tunatakiwa kumuombea kwa kila namna, kuimba nyimbo zote, kwa sauti yoyote, tucheze na kufanya lolote litakalokuwa na maana ya kuenzi kazi ya Mandela na mapinduzi aliyoleta.” Juzi, Rais Zuma alihudhuria misa ya maombezi katika Kanisa la Methodist ambalo hutumiwa na wazungu walio wengi jijini Johannesburg, wakati Rais mstaafu, Thabo Mbeki, aliungana na wananchi wengine katika masinagogi kumuombea Mandela.  Watu wengi wanadaiwa kujumuika katika Kanisa Katoliki lililopo mjini Soweto, ambapo walipokea wageni wengi kutoka London huku Askofu Caunterbury, Justin Welby Kiongozi wa Kanisa la Anglikana ambalo lina wafuasi takriban milioni 80 duniani.  Kabla ya kuzikwa, wafuasi wa Chama cha ANC watakuwa na kongamano la kuaga mwili wa Mandela, Desemba 14 litakalofanyika katika ngome ya kijeshi ya Waterkloof Air Force Base mjini Pretoria.** ** ** **Qunu****Katika Kijiji cha Qunu alikozaliwa Mandela, wananchi walikusanyika katika kanisa ambalo lilijengwa na mama yake Mandela miaka mingi iliyopita kumuombea.*** ***Askofu wa Kanisa hilo, Sabelo Ngqeleni, alisema: “Leo tunasherehekea kumbukumbu ya mtu muhimu katika Taifa letu.* ***“Lazima tulikumbuke kanisa hili ambalo muasisi wake ni mama wa Madiba, Noqaphi Nosekeni. Lilianza kutoa huduma mwaka 1960. * ***“Wakati sisi tukiendelea hapa, kule Mthataha watu zaidi 6,000 wamekusanyika ambako ni katika makazi ya Madiba.* ***“Vijana kwa wazee wamekusanyika kwenye viwanja vya Ngangelizwe ambako kumewekwa mahema, wakiwa wamevalia fulana zenye picha ya Madiba.* ***Mama mzazi wa Madiba alifariki dunia mwaka 1968.* **Mandela alifariki dunia Alhamisi iliyopita akiwa na umri wa miaka 95 huko Houghton, Johannesburg.****

Miaka 52 ya UHURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amewashauri watu wanaopanga kulipa kisasi pindi watakapopata madaraka kuachana na mawazo hayo.  Rais Kikwete ametoa ushauri huo wakati akitoa hotuba yake kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara, ambapo ameelezea mengi mazuri aliyoyafanya rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na kuwataka viongozi wa Tanzania kuiga mfano wa maisha yake ikiwa ni pamoja na kusamehe na kusahau bila kulipa kisasi.  “Najua kuna wengine hapa wamepanga kulipa kisasi, wanasema nikipata watanikoma.” Amesema rais Kikwete na kuwataka waache yaliyopita yapite na kuendelea kuganga yajayo, “acheni kulipa kisasi.” Rais Kikwete amesisitiza.  Hotuba ya Rais Kikwete ilijikita zaidi katika maisha ya mzee Nelson Madiba Mandela, katika kuungana na Afrika Kusini kuomboleza kifo cha kiongozi huyo shupavu na kutoa mfano wa jinsi viongozi wa Afrika wanapaswa kuiga mfano wa uongozi.

Saturday, 7 December 2013

Mradi wa DART waanza kuonyesha matunda

"*Basi la kwanza la mradi wa mabasi yaendayo kasi limewasili nchini na kuanza kufanya majaribio katika barabara zilizokwisha kamilika huku mengine yakitarajiwa kuwasili mapema mwaka kesho.*""* *""*Mtendaji mkuu wakala wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Bi Asteria Lambo amesema basi hilo ni miongoni mwa mabasi madogo yatakayoingia nchini yenye uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 40 na makubwa yatabeba abiria zaidi ya 150 na kuwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa na subira na kuwahakikishia mradi huo sio ndoto na adha ya usafiri itapungua mapema mwaka kesho.*"

Friday, 6 December 2013

Breaking News:Mzee Nelson Mandela (95) Amefariki Dunia

Habari za hivi punde zinajulisha kuwa; Raisi wa sasa wa Afrika ya Kusini ametangaza kwa masikitiko kuwa Mzee Nelson Mandela amefariki dunia tarehe 5 Desemba 2013majira ya saa 2:50 usiku ( kwa saaz a Africa Kusini) huko nyumbani kwake Johanesburg. Mzee t alikuwa kiongozi wa kwanza mweusi kutawala Africa kusini kama Raisi. Alitoka kifungoni mwaka 1990 na kuchaguliwa kuwa raisi mwaka 1994. Mwaka 1999 aliachia madaraka na mara ya mwisho kutokea kwente galaiki km kiongozi rasmi ilikuwa mwaka 2004. Inasemekana kifo chake kimetokana na maradhi ya mapafu yaliyokuwa yakimsumbua kwa kujirudia. Mungu ailaze roho yake pema Amen.