Thursday, 15 September 2016

BUSARA ZA BABA KWA BINTIYE

Msichana alinunua simu smartphone ambayo ni ghali mno. Baba yake alipoiona alimuuliza "Binti yangu uliponunua hiyo simu yako ya gharama cha kwanza kufanya kilikua ni nini?"

"Niliweka screen protector kuzuia michubuko ya kioo na nikanunua cover kwa ajili ya kuzuia ikianguka isichubuke" binti alijibu.

"kuna mtu alikusukuma kufanya hivyo?" baba alimuuliza bintie

"Hapana" binti alijibu

"Unafikiri huko si kuwatukana waliotengeneza simu kwamba hawakukamilisha kazi yao? Baba aliendelea kuuliza.

"Hapana baba" ni kwamba hata wanaotengeneza wanawakumbusha watu kuweka cover katika simu zao kuzuia kuharibika kwa urahisi"

"Je uliiwekea cover kwa vile simu ni bei rahisi na inamuonekano mbaya?" Baba aliendelea kusaili

"ukweli nimeiwekea cover sitaki iharibike mapema na ipoteze uthamani wake" binti aliendelea kumjibu baba yake.

"ulipoiwekea cover, imepunguza uzuri wa simu yako?"

"Hapana baba nafikiri ndio imeonekana nzuri zaidi tofauti na mwanzo, na imeipa simu yangu ulinzi ili isiharibike"

Baba akamwangalia binti yake kwa upendo na akamwambia, " Je kama nikikuomba ukave mwili wako ambao unathamani kubwa kuliko hata hiyo simu yako kwa nguo ndefu zisizo onyesha maungo yako kwa watu hovyo hovyo utafanya hivyo?"

Binti alibaki kimya!

Niambie! Wanaume waone maungo yenu wagundue nin?

Kwa unyenyekevu naomba niwe mkweli binti yangu, uvaaji wa nguo fupi na zisizo na staha ambazo zinaweka wazi maungo yenu obvious zinapunguza thamani yenu na heshima kwa jamii.

Watakaokutamani ni wanaume wakware tu wale wahuni wahuni! Ila mwanaume mwenye heshima zake hawezi akavutiwa nawe kwake atakuona kama msichana fulani wa kileo unayefaa kwa usiku mmoja tu na sio kwa maisha.

Cover your smartphone, cover your precious body for your husband only!

1 comment:

  1. Bonge la ujumbe lenye fundisho kwa mabinti...ahsante

    ReplyDelete

Maoni yako