Thursday 30 June 2016

USALAMA KUIMARISHWA VITUO VYA MABASI YAENDAYO KASI (DART)

Benjamin Sawe Maelezo

—————————–

Baadhi ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea katika baadhi ya vituo hivyo.

Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea abiria kuibiwa vitu vyao ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa.

Aliongezea kuwa walinzi wa kituo hicho wamekuwa wakifanya kazi ya kuwapanga abiria na kusahau majukumu yao ya kulinda usalama wa kituo hicho pamoja na mali zao.

“Tunashangaa hawa walinzi wanaolinda vituo hivi, abiria wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa nyakati za usiku lakini tunaona abiria wakiendelea kuibiwa sijui wahusika wapo wapi?”Aliuliza Bw. Ally.

Nae Bi. Herrieth Shangaa aliongezea kuwa licha ya vitendo vya wizi vinavyoendelea katika vituo hivyo kuna baadhi ya vitendo vikiwemo vya kujisaidia katika madaraja hayo hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msimamizi wa vituo hivyo ambae hakutaja kutajwa jina lake amesema kuna baadhi ya vituo ni vikubwa na wanawalinzi wachache hivyo wamejipanga kuongeza ulinzi ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa kidigitali wa kudhibiti wahalifu

Mradi wa mabasi yaendayo haraka ulioanza rasmi terehe 10, mei, 2016 umeonesha ni jinsi gani kero ya foleni itakavyopungua kwa kuwa mabasi hayo yanatumia njia yake ambayo ni miundombinu iliyojengwa kwa gharama kubwa sana.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako