Sunday 19 June 2016

NAULI ZA MABASI YAENDAYO KASI SASA WAWEZA KUTUMIA PLASTIK CARD

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Habari UDART, Deus Bugaywa
Na Dotto Mwaibale

MRADI wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (UDART) imeanzisha huduma kwa wateja wao za kutumia kadi maalumu wakati wa kupanda mabasi hayo itakayoanza rasmi leo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, David Mgwasa alisema wameanza kutoa huduma hiyo ya kadi ili kuwarahisishia wateja wao na kuondoa changamoto ya kusubiri tiketi kwa muda mrefu kabla ya kuondoka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya MaxMalipo ambao wameingia ubia na Udart katika matumizi ya kadi hizo, Mhandisi Juma Rajabu alisema kwamba kwa kuanzia wametoa kadi 200,000 ambapo kila kadi itauzwa kwa shilingi 5000 ingawa bei halisi kwa kadi moja ni shilingi 500 na sh.4500 inayobaki itakuwa ni malipo ya mteja wao.

“Shilingi 4500 zitatumika kama malipo ya nauli kwa siku saba hadi nane kwa kwenda eneo lolote na kuwa kadi hizo zitapatikana katika vituo vya Kimara, Mbezi, Morocco, Gerezani, Posta na kuwa zitakuwa ni endelevu” alisema Rajabu

Aliongeza kuwa katika nchi nyingi zimekuwa zikitumia kadi hizo katika kusafirisha abiria na kuwa kwa hapa nchini ni huduma mpya ambayo itakuwa na changamoto zake kabla ya kuzoeleka.
Alisema licha ya kuanzisha huduma ya kadi bado ile ya risiti itaenelea kama kawaida ambapo alisema namna ya kujiunga na hu duma hiyo unatakiwa kupiga *152*22#

No comments:

Post a Comment

Maoni yako