Saturday 4 June 2016

MAENDELEO YA MAKAZI AFRIKA; NIGERIA KUJENGA DUBAI YAO JIJINI ABUJA

Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula yupo nchini Nigeria kuhudhuria kikao cha Mkutano Mkuu wa 35 wa Shelter Afrique Jijini Abuja. Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 37 utakaofanyika nchini Tanzania mwaka 2018.
Mchoro huu juu na chini unaonyesha taswira ya mji wa kisasa unaotabiriwa kuwa Dubai ya Nigeria unaojengwa nje kidogo ya Jiji la Abuja ujulikanao kama Centenary City Abuja ambao wajumbe wa nchi mbalimbali za Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa 35 wa Shirika la Makazi Afrika waliweza kuutembelea na kujionea ndoto ambayo wanigeria wameamua kuitekeleza.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako