Thursday, 1 December 2016
TBL YAZINDUA MWONEKANO MPYA WA POMBE YA CHIBUKU KATIKA CHUPA
Watumiaji wa kinywaji maarufu cha nafaka kiitwacho Chibuku kinachouzwa sana katika Jiji la Dar, sasa watakuwa wakiburudika na kinywaji hicho kwenye chupa mpya ya ujazo wa nusu lita ambayo itauzwa kwa sh.700
SMARTPHONES ZINAVYOFIFISHA UTU NA UBINAAMU WETU
IT'S VERY SAD....hapa ndipo tulipofikia.Hivi karibuni mzee mmoja aliyekuwa na baskeli aligongwa AKIWA KATI YA BARABARA...Watu wanapiga PICHA huku wakitania...ATAKUWA AMEVUNJIKA KIUNO(mocking).. Huku wengine wakijipiga Selfie Badala ya Kumsaidia
Wednesday, 30 November 2016
KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE CHASITISHA UZALISHAJI KWA MUDA
UZALISHAJI katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara umesimama kwa muda kutokana na hitilafu za kiufundi zilizojitokeza katika mitambo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania, Harpreet Duggal alisema jana kwamba mafundi wa Dangote wapo kazini na shughuli za uzalishaji zitarejea katika siku chache zijazo.
Alisema kiwanda kinachomilikiwa na bilionea namba moja Afrika, Alhaji Aliko Dangote wa Nigeria kilianza uzalishaji wa kibiashara mwaka huu na kama ilivyo kwa kiwanda kingine kama hicho, jambo lolote linaweza kutarajiwa hasa katika miezi ya mwanzo.
Alisisitiza, “hitilafu hizi ni za kawaida na uzalishaji utarejea katika kipindi kifupi kijacho.”
Akizungumzia gharama za uzalishaji, Duggal alisema uendeshaji nchini uko juu huku miongoni mwa sababu ikiwa ni matumizi ya jenereta za dizeli katika kuendesha kiwanda.
Hata hivyo, alisema serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya kutafuta njia ya kuwapunguzia mzigo.

MTOTO WA DIAMOND PLATNUMZ
Hakuna ubishi kuwa Princess Tiffah ndiye mtoto maarufu zaidi Afrika kwa sasa.
Umaarufu wake unazidi kuongozeka kiasi ambacho wiki hii amefikishafollowers milioni 1 kwenye mtandao wa Instagram.
Ila katika nchi hii hii wapo watoto wengine wanaishi hivi

Tuesday, 29 November 2016
NDEGE ILIYOBEBA WACHEZAJI WA BRAZIL YAPATA AJALI
Habari za kusikitisha katika ulimwegu wa soka ni kwamba, klabu ya Chapecoense ya Brazil imepata ajali baada ya ndege iliyokuwa imebeba wachezaji pamoja na viongozi kuanguka kwenye mji wa Medellin, Colombia.Chapecoense ilikuwa imefika hatua ya fainali ya Copa Sudamericana, ambayo ni sawa na Europa League kwa Ulaya na walikuwa wanaelekea Medellin kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa fainali dhidi ya Atletico Nacional siku ya Jumatano.
Habari za hivi punde zaeleza kuwa abiria 71 waliokuwa katika ndege hiyo wamefariki ila kuna wachache wanaosadikiwa 6 walionusurika kifo

MARAIS WA TANZANIA NA ZAMBIA WAAZIMIA KUBORESHA ZAIDI TAZARA NA TAZAMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu tarehe 28 Novemba, 2016 wamekubaliana kuchukua hatua za haraka na madhubuti kuboresha utendaji kazi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA ili miradi hiyo miwili ilete manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi Tanzania na Zambia.
Monday, 28 November 2016
MBEYA YA PILI AFRIKA KWA WINGI WA MADHEHEBU
Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, jiji hilo lina makanisa 450 na Mtaa wa Sae pekee una madhehebu tisa huku Mtaa wa Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.
Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa Kanisa la International Evangerism Assemblies of God, amesema migogoro ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.
Meya huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.
Amesema madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.
“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo

UGENI WA MARAISI WAWILI NCHINI TANZANIA WIKI HII
Rais Magufuli leo amepokea Marais wa Mataifa mawili ya Tchad na Zambia kwa mialiko ya ziara za kikazi.Rais wa Chad Idriss Deby atakuwepo nchini kwa siku mbili katika ziara ya Kikazi; wakati rais wa Zambia mhe. Edgar Lungu atakuwepo kwa siku 3
Subscribe to:
Posts (Atom)