Thursday, 19 December 2013

Tulikotoka ni mbali

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mama huyu naona kaamua kumwonyesha mwanae maisha yalivyo Watoto hawa pia japo wafurahia mazingira ya nyumbani ila pia wanajiandaa kuwa wanamichezo wazuri hapo baadae. Muhimu ni kukuza tu vipaji vyao Huyu nae ametokelezea kivyake alivyokuwa anacheza. Ama kweli nyumbani raha

Wednesday, 18 December 2013

Mv.MAGOGONI chapata kizaazaa leo

Kivuko kikubwa cha MV Magogoni leo kimekwama katikati ya bahari katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na hitilafu za kiufundi.Pantoni hilo linafanya safari kati ya Kigamboni na Magogoni, Dar es Salaam. Kiini cha kizaazaa hicho bado hakijafahamika, ila mashuhuda wanasema  Kivuko kilipoteza mwelekeo majini  kikiwa na abiria na magari baada ya injini zake kushindwa kufanya kazi. *" Juu abiria wanaonekana wamevaa "life jackets" ikiwa itatokea kupiga mbizi au la. Chini ni mv.Magogoni inavyoonekana ktk safari zake kawaida

Ndege ya shirika la Ethiopian Airline yatua Arusha kwa dharura

Habari iliyoifikia hivi punde toka jijini Arusha, inaeleza kuwa Ndege ya abiria aina ya Boeing 787 ya shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) mchana huu imeshindwa kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutoka na hitilafu iliyokuwepo Uwanjani hapo na kulazimika kutua kwa dharula kwenye Uwanja wa Mdogo wa Arusha,hali iliyopelekea Ndege hiyo kusimama nje kabisa ya uwanja huo huku abiria zaidi ya 200 wakiwa ndani ya ndege hiyo mpaka sasa bila ya kushuka.**** ****Wataalam wa Ndege wapo eneo la tukio hivi sasa kutafakari namna watakavyoweza kuwashusha abiria hao na kutafuta namna ya kuweka sawa mambo ili Ndege hiyo iweze kuruka.**** ****Tuinaendelea kufatilia kwa ukaribu tukio hilo, na tutaendelea kufahamishana kadri taarifa zitakavyokuwa zinakitufikia.* * **PICHA NA MDAU WETU KUTOKA ARUSHA*

Sudan Kusini hali si shwari

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, anasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua jaribio la mapinduzi, baada ya usiku mzima wa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba. Bw. Kiir, anayetoka katika kabila kubwa zaidi la wa Dinka amewatupia lawama wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wake Riek Machar, anayetoka katika kabila dogo la Nuer. Aidha Kiir ametangaza amri ya kutotembea usiku mjini Juba na kusema serikali sasa inaudhibiti mji huo. Makundi hasimu ya wanajeshi walipigana vikali kwa saa kadhaa na kuna ripoti za kuwepo majeruhi maelfu wakiripotiwa kukimbilia usalama wao. Milio ya risasi sasa inaripotiwa kupungua. Kumekuwa na hali tete ya kisiasa nchini Sudan Kusini tangu mwezi Julai wakati Rais Kiir alipovunja na kuwafuta kazi mawaziri wote katika baraza lake akiwemo Makamu wa Rais Bw.Machar.(P.T)

Tuesday, 17 December 2013

HUTUFANANI

*Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharoosi 'Malkia wa Nyuki'.*"MLEZI wa Simba, Rahma Al Kharoosi, ametua jijini Dar es Salaam akiwa kwenye ndege kubwa yenye uwezo wa kubeba watu 150, lakini yeye akiwa ndiye abiria pekee ndani ya ndege hiyo. Rahma, maarufu kama Malkia wa Nyuki, ametua na ndege hiyo aina ya Airbus 320 inayomilikiwa na Serikali ya Oman na anaitumia yeye kupitia cheo chake cha Balozi wa Heshima wa Oman nchini Morocco. Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu 17, kati ya hao 16 ni wafanyakazi ndani ya ndege ambao ni daktari mmoja, walinzi wanne, waliobaki ni marubani na wahudumu. Akizungumza dakika chache kabla ya kuondoka nchini jana, saa 10 alfajiri, Malkia wa Nyuki alisema alishuka nchini kwa ajili ya mapumziko ya siku moja, pia kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Simba. “Nimepita tu, tumepumzika kidogo hapa na baada ya hapo ninakwenda Comoro kwa ajili ya kuzungumza na kumchukua Rais wa Comoro. “Lakini wakati wa mapumziko, nimepata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya viongozi wa Simba kuhusiana na mwenendo wa timu kwa hivi sasa. “Kwa sasa namaliza majukumu yangu kikazi halafu nitarudi tena safari nyingine nchini kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo na viongozi wenzangu wa Simba ili tujue tunaweza kufanya nini kuendelea kurekebisha mambo,” alisema. Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Malkia wa Nyuki alisindikizwa na mwanaye Fatma, maarufu kama Nyuki Mtoto na watu wengine wawili. Baada tu ya yeye kupanda ngazi za ndege hiyo, walinzi na wafanyakazi waliokuwa nje ya ndege hiyo nao waliingia na ikaanza safari kwenda Comoro.CHANZO GPL

Sunday, 15 December 2013

Hatimaye Mandela azikwa huko Qunu

Leo ndio siku ya mazishi ya Mwana wa Mama Afrika, Nelson Rolihlahla Mandela. Anazikwa kijijini kwao Qunu. Mandela anayetoka kwenye kabila la Xhosa alizaliwa Julai 18, 1918 kijijini Mvezo, kando ya mto Mbashe, Wilaya ya Umtata, Makao Makuu ya Jimbo la Transkei. Ukoo wa Mandela una mahusiano na Ukoo wa Kifalme wa Thembu. Baba yake Mandela, Gadla Henry Mphakanyiswa alikuwa Chifu kwa damu na kwa desturi. Naye akathibitishwa kuwa Chifu wa Mvezo na Mfalme wa himaya ya Thembu. Mandela mwenyewe alizaliwa na jina Rolihlahla, ikiwa na maana ' Mwenye kuvuta matawi ya miti'. Na kwa lugha yao ina maana ya ' Msumbufu'. Na hakika, Mandela amekuwa ' Msumbufu' kwa utawala wa kibaguzi hadi pale waliposalimu amri. Mandela anasimulia, kuwa kumekuwa na hekaya sizizo za kweli kwenye kabila lao, kuwa naye ( Mandela) alikuwa mmojawapo katika mlolongo wa kurithishwa Uchifu kwenye himaya ya Thembu. Kwamba ingefika wakati naye Mandela angetawazwa kuwa Chifu. Mandela analikanusha hilo, anasema;(P.T) Juu mwili wa Mandela ukiwa juu ya kaburi tayari kuzikwa. Chini ni mama Vicky Swai(aliyetunza viatu vya Mandela akiwa Tanzania) na mama Maria Nyerere katika mazishi ya Mandela huko Qunu

Mandela Rafiki wa kweli wa Tanzania:Raisi Kikwete

HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KWENYE MAZISHI YA MANDELA YAGEUKA GUMZO, WAAFRIKA WASEMA NI HOTUBA BORA BAADA YA ILE YA BARACK OBAMA KWENYE UWANJA WA FNB  Hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kwenye mazishi ya Rais wa kwanza wa Afrika Kusini Nelson Mandela leo huko Qunu, Eastern Cape nchini Afrika Kusini, imewakumbusha Waafrika ukaribu wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Katika hotuba hiyo iliyosifiwa na Waafrika wengi, Kikwete aligusia jinsi ambavyo Afrika Kusini haipo peke yake kwenye maombolezo ya shujaa wao, Mandela. “Watu wa Tanzania wangependa mjue kuwa hamko peke yenu. Watakuwa nanyi katika kipindi hiki cha maombolezo na baada ya hapa. Potezo lenu ni potezo letu. Alikuwa kiongozi wetu, shujaa wetu, mfano wetu, baba yatu kama alivyo kwenu.” “Watu wa Tanzania wamepoteza rafiki mkubwa. Komredi mkubwa wa jeshi.” Katika hotuba hiyo pia, Kikwete alikumbushia jinsi Nelson Mandela alivyoacha viatu vyake jijini Dar es Salaam mwaka 1962 ambavyo vilirudishwa kwake alipokuja kuwa rais. "Ulikuwa ni muendelezo mwingine wa kuvutia wa ujio wake Tanzania mwaka 1962," alisema. "Katika kuufanya ujio wake kuwa makini, hakukaa kwenye hoteli. Alikaa kwenye nyumba ya Cyril Swai. "Alipoondoka, aliacha viatu vyake kwa matumaini kuwa akiwa anarudo angevipitia viatu vyake Bahati mbaya hakupitia Dar es Salaam tena sababu aliporejea Afrika Kusini alikamatwa na kukaa jela miaka 27. Bahati nzuri, familia ya Swai ilivitunza viatu vyake na mwaka 1995, viatu hivyo vilirudishwa kwake.”

Saturday, 14 December 2013

Familia ya Nyerere yatuma wawakilishi Qunu kwenye mazishi ya Mandela

Familia ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere itawakilishwa katika mazishi ya Rais wa Kwanza Mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, ambaye atazikwa kesho katika Kijiji cha Qunu, Mthatha Jimbo la Eastern Cape. Habari ambazo gazeti hili lilizipata jana mjini Pretoria zinasema kuwa Mama Maria Nyerere, ambaye ni mjane wa Baba wa taifa, alialikwa kuhudhuria mazishi hayo kwa kuzingatia uhusiano uliopo baina ya familia hizo mbili. Hata hivyo, imethibitika kuwa Mama Maria hataweza kuhudhuria mazishi hayo kesho, badala yake amewatuma wawakilishi ambao ni mabinti zake wawili; Anna Nyerere ambaye ni mtoto wa pili na mtoto wake wa saba, Rosemary Nyerere. Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa sita wa Mwalimu alithibitisha jana kwamba familia yao imealikwa kushiriki mazishi hayo, lakini akaweka wazi kwamba: "Mama hataweza kwenda kuzika, atakwenda baadaye kidogo baada ya mazishi kufanyika." Madaraka alisema kwa jinsi afya ya mama yake ilivyo sasa, hataweza kwenda Qunu. "Kwa kawaida mazishi haya ya kitaifa huwa yana mambo na pilika nyingi, kwa hiyo mama ameona asubiri," alisema. Kuhusu kifo cha Mandela, Madaraka alisema kwamba kama wanafamilia, wameguswa na msiba huo na kuwa kimewakumbusha uchungu walioupata wakati walipofiwa na baba yao Oktoba 14, 1999. "Kwa kweli tumeguswa sana na msiba na tunawapa pole sana, tunakumbuka kwamba wakati baba alipofariki, Mama Graca tulikuwa naye, alikuja kabla ya mazishi na alikuwepo kwenye mazishi na baada ya mazishi aliendelea kukaa kwa siku kama saba," alisema Madaraka na kuongeza: "Pia tunakumbuka kwamba Mzee Mandela yeye alikuja baadaye mpaka Butiama kutoa pole. Ilikuwa Novemba 26, 1999 kwa hiyo tunaguswa na msiba huu." Awali, gazeti hili lilidokezwa kwamba watoto hao wa Nyerere walikuwa wamefikia katika Hoteli ya Burgers Park, Pretoria lakini walipotafutwa katika hoteli hiyo wafanyakazi walisema kwamba tayari walikuwa wameondoka. Chanzo:Mwananchi

Friday, 13 December 2013

SIMPLE MIND

Wife:. Honey, before we got married , you used to buy me gifts and expensive jewellery.. Husband:. Yes... So?? Wife:. How comes you dont do it anymore?? Husband:. Have you ever seen a fisherman giving worms to the fish he has already caught???

Ukweli kuhusu Filamu za Kibongo

Bila wasichana warembo kwenye filamu ya kibongo, hakuna atakayeinunua na huenda waandaaji wakaishia kuiangalia tu nyumbani na familia zao Kwa mujibu wa Tino, wasichana warembo ni ‘chambo’ kinachowavuta wanunuzi wa filamu za Tanzania. Ujuzi wa uigizaji na kipaji, si sababu kwao. Akiongea na gazeti la Mwanaspoti, Tino alisema warembo hao pamoja na kuzifanya filamu zivutie pia huwa na juhudi katika kazi hiyo tofauti na wanaume na wanaipenda kazi yao. “Kwa kweli bila kuweka wasichana warembo katika filamu yako hutauza kwa sababu wengi wana juhudi za kufanya mambo mapya kila kukicha, lakini pia wanakuongezea mvuto kwa kuwa warembo ni kama maua,”alisema Tino. Pengine ndio maana waigizaji wa kike wanaotamba ni walewale akina Wema Sepetu, Lulu, Irene Uwoya, Jacky Wolper, Batulli na wengine waliojaaliwa sura za kuvutia