Huu sijui unaitwaje Mdako Bao Michezo hii inawajengea watoto tunu njema nyingi kama umakini, utulivu, furaha, urafiki, ubunifu, kuchemsha bongo, kutulia nyumbani na mengine mengi. Yafaa kuendelezwa
Tatizo la usafiri linalopelekea kujazana kwenye vyombo rasmi na visivyo rasmi vya usafiri kimakosa na hivyo kuhatarisha maisha. Hii si kwetu tu,hata kwa wenzetu, ila si kwamba tunahalalisha hili!
MwanaBlog anatoa shukrani za pekee kwa wote wanaoendelea kumfariji katika kipindi hiki kigumu akiwa nchi za mbali na hivyo kushindwa kuhudhuria mazishi ya baba mpendwa.Asanteni sana na Mungu awakarimu.
Mpendwa Mzee Amedeus Mwangoka,Baba mzazi wa mwenye Blog hii ametutoka ghafla Kibosho Hospital-Moshi, usiku wa Jumatatu 23/03/2009. Mazishi yanafanyika leo Jumamosi 28/03/2009 nyumbani Kilingi-Sanya Juu Kilimanjaro. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina la Bwana libarikiwe. Apumzike kwa Amani.Amina.
Paradise Holiday Resort pamoja na Ocenic Bay zote zikiwa Bagamoyo zachomeka na moto mkubwa. Kwa mujibu wa shuhuda wetu moto huo ulianza eneo la Bistro Alakat Restaurant ambapo cheche za moto ziliwaka hadi kwenye makuti. Moto ukaenea kwenye Main Restaurant iliyo karibu na store ya chakula. Moto huo ulienea hoteli nzima na ikawa vigumu kuuzima. Magari ya zima moto yalichelewa kufika eneo la tukio kwa sababu yanatokea Dar es salaam. Hoteli hii ya kifahari imeteketea kabisa kilichobakia ni vibanda vitatu vya makuti katika eneo la bahari, Paradise Holiday Resort ilikuwa na vyumba tisini na tano. Moto huwo huo pia umeathiri Hoteli ya jirani ya Oceanic Bay, kiasi cha hasara hakijajulikana mpaka sasa.
Unaondokea katika Jiji maarufu kama hili Unachukua usafiri wa basi hapa kuelekea Airport Unapita Barabara hii kuelekea Airport Unaingia katika kiwanja hiki au hiki cha ndege Unachukua usafiri wa Ndege kama hii Unapokaribia Nyumbani Tanzania, unaona mandhari safi ya Jiji la Dar-es-Salaam Unashukia katika kiwanja chetu cha ndege Unachukua usafiri huu kuelekea katikati ya Jiji kujipumzisha kwa muda kabla ya kuelekea kijijini kwa Babu na Bibi Unajipumzisha katika moja ya sehemu kama hii Unatembelea sehemu kama hizi kabla ya kuondoka, huku ukituma usafiri kama huu Halafu unaondoka kuelekea Ubungo Bus Terminal kwa usafiri huu au huu Safari ya kuelekea Kijijini toka Jijini inaanza hapa Vijijini unapokelewa na usafiri kama huu kuelekea makazi asilia UNAPOTEMBEA KUELEKEA NYUMBANI UNAPISHANA NA WANAKIJIJI WENZIO WANAOTESA KWA RAHA ZAO KIVYAOVYAO
Mpenda nyumbani nimeamua kuungana nanyi kuwaletea blog hii maalum inayowapa habari za nyumbani Tanzania na habari toka sehemu mbalimbali lakini zenye lengo la kuelimisha,kukosoa,kupongeza na kuburudisha jamii. Karibuni Nyumbani!