Wednesday, 16 August 2017

BODABODA MARUFUKU KUBEBA WATOTO NA WANAFUNZI CHINI ZA MIAKA 10

Jeshi la Polisi August 15, 2017 limetoa tamko la kupiga marufuku Waendesha Bodaboda kubeba watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 na kwamba atakayekiuka agizo hilo pamoja na mzazi aliyeruhusu mwanawe kubebwa watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na faini, kifungo au vyote viwili.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye pia ni Afisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Theopista Malya, amesema kuwa watoto wamekuwa kwenye hatari kubwa wakipandishwa kwenye Bodaboda na wakati mwingine waendesha bodaboda hubeba watoto zaidi ya mmoja jambo ambalo ni lazima likemewe.

Aidha, alisema kuwa Jeshi hilo limeandaa kipindi maalumu cha Radio kitakachorushwa na Clouds FM kila siku ya Jumatano saa 2:00 Usiku kikiwa na lengo la kuongeza elimu kwa waendesha Bodaboda katika kuzingatia Usalama Barabarani pindi wanapofanya shughuli zao.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mabalozi wa Usalama barabarani (TSA), John Seka alisema kipindi hicho kitalenga kuwapa elimu waendeshaji wa bodaboda.

Pia, alitumia nafasi hiyo kuwataka wafuate sheria zilizowekwa na Sumatra ili waepukane na mkono wa sheria.

Paulina Shayo ambaye ni mwakilishi kutoka WAT Saccos alisema kuwa wanatoa mikopo kwa bodaboda na kwamba mikopo hiyo itawasaidia kuwa wamiliki halali wa vyombo hivyo.

Sunday, 30 July 2017

Sunday, 23 July 2017

HABARI NJEMA. CCM KUTOA MIKOPO KWA WANAFUNZI YATIMA VYUO VIKUU

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wake, Humphrey Polepole kimetangaza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambao wamekosa mikopo ya kuendelea na masomo na wanafunzi ambao ni yatima.

Taarifa iliyotolewa na Polepole inasema kuwa wanafunzi hao wanapswa kufika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kusaidiwa shida zao hizo za mikopo, jambo ambalo limepokewa tofauti na baadhi ya watu wakidai kuwa suala la kutoa mikopo kwa wanafunzi ni jukumu la bodi ya mikopo.

Kutokana na mitazamo ya watu kuwa tofauti katika jambo hili, Humphery Polepole aliibuka na kusema kuwa upinzani wa Tanzania ni mtihani mkubwa kwani wanapojaribu kutatua matatizo ya watu wanakujua juu na wasipotatua matatizo pia wanakuja juu.

"Tukikaa kimya kwa shida za watu inakuwa tatizo, tukishughulika na shida za watu inakuwa tatizo kubwa. Huu upinzani mtihani" alisema Polepole

POLENI KWA BLOG YENU KUTOKUWA HEWANI MUDA

Wapendwa wanablog ya Karibu Nyumbani, kwa takribani wiki 4 hivi Blog yenu haikuwa hewani kutokana na Safari ya Kikazi sehemu ambapo upatikanaji wa Internet ulikuwa mgumu. Karibuni tena.

Monday, 26 June 2017

EID MUBARAK

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) pampja na Viongozi mbali mbali wa Dini na Mashekhe wa Dini ya Kiislamu waliofika Ikulu Mjini Unguja leo kumtakia Rais Sikukuu njema baada ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan,wakiitikia Dua Iliyoombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibae Sheikh Saleh Omar Kabi,(wa pili kushoto),[Picha na Ikulu.] 26/06/2017.
Alhaj Mzee Ali Hassan Mwinyi akiongoza Swala ya Eid kuadhimisha sikukuu ya Eid el Fitr
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakichukua Chakula wakati wa hafla fupi ya Futari iliyoandaliwa na Benki ya Azania na kufanyika ofisi za Bakwata mkoa wa Kilimanjaro

Sunday, 25 June 2017

HONGERA RAYVANNY WA WCB

Msanii wa Bongo Flava, Rayvanny kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) ameshinda tuzo ya BET (Black Entertainment Television) kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act Artist’.

Kufuatia ushindi huo msanii Diamond Platnumz ambaye anaiongoza WCB amepongeza ushindi huo wa Rayvanny, amesema kuwa zaidi ya miaka mitatu tunaenda na kurudi patupu lakini safari hii si patupu tena kufuatia ushindi huo.

“Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah! ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale”

Saturday, 24 June 2017

TAARIFA YA SIKUKUU YA EID EL FITR


Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akiwa katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo

Thursday, 22 June 2017

SHOPPING ZA EID IMEPAMBA MOTO

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya Mfungo wa Ramadhani kuisha, maeneo mengi ya masoko yamejaa wateja wakifanya manunuzi kwa ajili ya kupendeza wakati wa Sikukuu ya Eid.
Nawatakia wote maandalizi mema

WATAKAOPATA MIMBA SHULENI KUKIONA CHA MOTO

Rais John Magufuli amesema wakati wa utawala wake hakuna mwanafunzi atakayepata mimba na kuruhusiwa kurudi shule.

Ameyasema hayo leo (Alhamisi) wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani Pwani ambako amezindua viwanda saba.

“Azae halafu aende kuwahubiria wenzake, unajua ilikuwa hivi, halafu nilifanya hivi,”amesema.

Amesema waliozaa shuleni wanaweza kwenda kupata elimu nyingine kama vyuo vya ufundi stadi (Veta) na kilimo badala ya kurudi shule na kuanza kuwafundisha wenzao yale waliyoyafanya.

“Mnataka niwaambie warudi shule halafu, ni bora wakalime ili ile nguvu waliyoitumia kujifungua waitumie kulima,” amesema.

Amesema; “Ni rahisi zaidi kuzalia chuo kikuu, ule mwaka wa kwanza, wa pili lakini sekondari, darasa la kwanza kupeleka walio na watoto, tunapoteza maadili yetu, watazaa mno.”

“Mtajikuta darasa la kwanza wote wanawahi nyumbani kwenda kunyonyesha. Hii tutalipeleka Taifa pabaya,” amesema

Mhe RAIS MAGUFULI AFUTARISHA KIBAHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kunawa na kisha kuchukua chakula leo Jumatano Juni 21, 2017 katika futari aliyowaandalia wananchi wa mkoa wa Pwani katika Ikulu ndogo ya Kibaha ambayo ilihudhuriwa pia na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry pamoja na viongozi wengine wa dini, serikali, vyama na watoto wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali vya yatima mkoani humo