Wednesday, 17 February 2016

UGANDA: MHE RAIS MUSEVENI AWANIA AWAMU YA TANO MFULULIZO

Rais Yoweri Museveni aliwahi kusema kuwa viongozi wanaokaa sana madarakani ndiyo walikuwa chimbuko la matatizo ya Afrika, lakini miaka 30 baadae, Museveni anatazamia kuingia muongo wa nne madarakani nchini Uganda.
"Wale wanaosema, 'aende,' wanahitaji kufahamu kuwa huu siyo wakati sahihi," Museveni alisema wakati wa mmoja ya mikutano yake ya kampeni hivi karibuni kuelekea uchaguzi mkuu wa Februari 18 ambao wengi wanataraji atashinda. "Mzee huyu ameiokoa nchi hii, vipi unamtaka aondoke? Ninaweza kuondoka kwenye shamba la migomba niliopanda na ambayo imeshaanza kuzaa matunda?"
Museveni alifanikiwa kubadilisha katiba mwaka 2005, na kuondoa ukomo wa mihula miwili. Viongozi wengine wa Afrika wamefuata nyayo zake, wakibadili au kurekebisha sheria ili kusalia madarakani, wa karibuni zaidi wakiwa marais wa Burundi Pierre Nkurunziza na wa Rwanda Paul Kagame.
Kwa sasa, Museveni hana nia ya kukabidhishi madaraka kwa mtu yeyote, akipinga ukosoaji wa mataifa wahisani ya magharibi kuhusiana na kukithiri kwa rushwa na hatua za kutoa madaraka makubwa kudhibiti mashirika ya kiraia na yale yasiyo ya kiserikali.
Wakati akiwania kuingia muongo wake wa nne madarakani, Museveni anaednelea kuwa mmoja wa viongozi wajanja na ving'ang'anizi zaidi barani Afrika, sambamba na wengine mifano ya Jose Eduardo dos Santos wa Angola na Teodoro Obiang wa Guinea ya Ikweta (wote wako madarakani tangu 1979), Robert Mugabe wa Zimbabwe (tangu 1989) na Paul Biya wa Cameron (tangu 1982).
Kwa sehemu kubwa, Uganda imekuwa na amani wakati wa utawala wa Museveni. Uasi wa kaskazini, unaoongozwa na kichaa wa miujiza Joseph Kony na kundi lake la Lord's Resistance Army (LRA), ulifurushwa nje ya nchi hiyo muongo mmoja uliyopita na mkono wake imara umezuwia machafuko ya kutumia silaha na ugaidi.
Hali ya uchumi iliboreka na Uganda ilishuhudia ukuaji wa asilimia 7 katika miaka ya 1990 na 2000, ukisukumwa na uwekezaji wa umma katika miundombinu na kufufuka kwa kilimo. Pia aliendesha kampeni yenye ufanisi dhidi ya maradhi ya ukimwi na maambukizi yake.

"MIMBA ZA UTOTONI"

FIRST LADY MAMA JANETH MAGUFULI ATEMBELEA SHULE YA MBUYUNI KUWASALIMU NA KUWAAGA RASMI


LEO Feb 17 2016, Mke wa Rais John Pombe Magufuli Janeth Magufuli amewasili katika shule ya msingi Mbuyuni, Dar kwa ajili ya kuagana na walimu wenzake pamoja na wanafunzi aliokuwa akiwafundisha

Shule ya Msingi Mbuyuni ni shule ambayo Mama Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza na baadaye mwaka 1995 kurudi tena kufundisha hapohapo kwa miaka 17 hadi mumewe Rais Magufuli alipochaguliwa kuwa Rais wa Tanzania.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi ya saa toka kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi ya Mbuyuni, Mwalimu Dorothy Mwalecela , Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni katika hafla hiyo leo
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa ameketi kwenye meza yake katika ofisi ya waalimu katika shule ya Msingi ya Mbuyuni, Oysterbay, jijini Dar es salaam wakati wa sherehe fupi ya kuwaaga rasmi walimu wenzake na wanafunzi wa shule hiyo ambayo ana historia nayo ndefu sana kwani ndipo yeye mwenyewe aliposomea elimu ya msingi toka darasa la kwanza hadi la saba kabla hajarudi tena hapo kama mwalimu na kufanya kazi kwa miaka 17 mfululizo.

Tuesday, 16 February 2016

MBWA MWITU HIFADHI YA SERENGETI WAANZA KUONGEZEKA

Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe amepongeza jitihada zinazofanywa na watafiti kwa kurudisha mbwa mwitu katika Hifadhi ya Taifa Serengeti baada ya kutoweka katika miaka ya tisini. Waziri Maghembe alitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki alipokuwa akiachia huru kundi la sita la mbwa 11 waliokuwa wamehifadhiwa katika boma maalum ili kurejea katika makazi yao ya asili.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe (MB) akiongea wakati wa tukio la kuachia huru kundi la sita la mbwa mwitu 11 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi sita kwenye boma maalumu la mradi wa mbwa mwitu

SIMANZI: MWANAMUZIKI JOHN WOKA AFARIKI DUNIA

Akiongea kwa simu kaka wa marehemu Omari Milay, amesema walipigiwa simu alfajiri ya leo na kujulishwa kuwa John Walker amefariki katika hospitali ya Muhimbili, alipokuwa akipata matibabu ya ajali aliyopata siku ya jana.

John Wolker alipata ajali ya kugongwa na kitu kizito kwenye paji la uso, alipokuwa garage maeneo ya Sinza akitengeneza gari yake, kwa bahati mbaya mtungi wa gesi ukalipuka na moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani,
Tarifa za awali za madaktari zilisema wanahofia kipande hiko kimefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.
Mipango ya mazishi familia imesema inakutana kujadili na mara itakapokamilika watajulisha watu nini kinaendelea.
Msanii John Wolker ambaye alikuwa kwenye kundi la Watukutu Family, alijipatia umaarufu kwa nyimbo zake za Sophia, Baby Gal na nyinginezo, ambazo aliziimba kwa mtindo wa mlevi

UPANUZI WA BARABARA YA MWENGE - MOROCCO WAENDELEA VIZURI


Sehemu ya Barabara ya Morocco kwenda Mwenge ikiwa katika hatua ya kutolewa tabaka ya udongo wa chini na kuwekwa tabaka ya udongo mpya kama inavyooenekana katika picha leo jijini Dar es Salaam .
Kipande cha Barabara ya Mwenge-Morocco kilicho kamilika kwa kiwango cha lami katika eneo la Mwenge-Bamaga kinavyoonekana katika picha

Monday, 15 February 2016

WAZIRI WA MFANO MHE: UMMY MWALIMU

Baada ya Mhe.Rais Magufuli kuagiya jengo moja la Utawala katika Hospitali ya Muhimbili ligeuzwe wodi ya Kinamama Wazazi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu amekuwa wa MFANO alipojiunga na watumishi wenzie kuhamisha na kufanya usafi katika Jengo hili. Kweli utumishi mzuri ni ule wa kuwa Mfano.
Mhe Waziri Ummy Mwalimu akishiriki kufagia ndani ya Jengo hilo
Mhe.Waziri Ummy Mwalimu akisaidiana na mtumishi mwingine kwenda kumwaga takataka
Tayari wagonjwa wameanza kutumia jengo hilo

AGIZO LA MHE.RAIS MAGUFULI YAANZA KUTEKELEZWA MUHIMBILI

AGIZO la Rais John Magufuli la kuibadilisha jengo la maofisa wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto lililopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, limetelekezwa baada ya jana maofisa hao kuondoa vifaa vyao.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akipokea vifaa kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa yaTaifa Lauren Rugambwa Bwanakunu vitakavyotumika katika wodi ya Afya ya uzazi ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Hospitali ya Muhimbili Prof Lawerence Mseru na nayefata ni katibu Mkuu wa wizara hiyo Mpoki Ulisubisya
Mafundi wakifunga vitanda katika jengo hilo

MHE:RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MABALOZI § NA WATUMISHI WENGINE SERIKALINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.

Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.

Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:

Naibu Kamishna wa Polisi Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi, na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.

Naibu Kamishna wa Polisi Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.

Naibu Kamishna wa Polisi Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia.

Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni.

Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.

Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
15 Februari, 2016

VALENTINE IMESHAPITA SASA TURUDI KAZINI KUIJENGA NCHI NA SISI WENYEWE

Wafanyabiashara hawa wameonyesha kupenda sana kazi yao hasa kwa utanashati. Biashara yahitaji mazingira mazuri ya mfanyabiashara ili kuvutia wanunuzi. Pigeni kazi kina kaka.