Sunday, 24 May 2015

NAWATAKIA JUMAPILI NJEMA NA MAPUMZIKO MEMA YA MWISHO WA WIKI

Watoto hawa wanahitaji kupata matumaini ya maisha mema mbeleni. Tuwasaidie wafikie ndogo hiyo nzuri

Saturday, 23 May 2015

MAPACHA WAOLEWA NA MWANAUME MMOJA

Owami na Olwethu Mzazi,mapacha wenye umri wa miaka 26 ,kutoka Vosloorus ,Afrika Kusini, hivi karibuni wamefunga ndoa na mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Mzukiseni Mzazi mwenye miaka 51.
Walipoulizwa na jarida moja nchini Afrika Kusini ,kwanini wameamua kuolewa na mwanaume mmoja,mapacha hao walisema wamekuwa wakishare kila kitu tangu walipokuwa na umri mdogo.

“ Siku zote tumekuwa tukifanya kila kitu pamoja. Tuna share kila kitu. Hivyo ndivyo bibi yetu alivyo tulea. So tulipo fikiri kuhusu kuolewa, tuliweka dhamira kuwa, mwanaume yoyote atakaye taka kumuoa mmoja wetu,lazima atuoe wote wawili. Owami ali lieleza jarida la Drum,la nchini Afrika Kusini.

WASHINDI TUZO ZA WATU

Hii ni orodha kamili ya washindi
Mtangazaji wa redio anayependwa
D’Jaro Arungu – TBC FM

Kipindi cha redio kinachopendwa
Papaso – TBC FM
Mtangazaji wa runinga anayependwa
Salim Kikeke – BBC Swahili
Kipindi cha runinga kinachopendwa
Mkasi – EATV
Blog/Website inayopendwa
Millardayo.com

Muongozaji wa video anayependwa
Hanscana
Muongozaji wa filamu anayependwa
Vincent ‘Ray’ Kigosi

Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa
Wema Sepetu
Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa
Hemedy PHD
Mwanamuziki wa kike anayependwa
Lady Jaydee
Mwanamuziki wa kiume anayependwa
Alikiba
Filamu inayopendwa
Kigodoro
Video ya muziki inayopendwa
Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz

MBIO ZA URAISI OKTOBA

Thursday, 21 May 2015

KITUO CHA KUCHAKATA GESI KINYEREZI - 1 DAR KUKAMILIKA MWAKA HUU

Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.

“Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi Jilima.

YALIYOJIRI MAGAZETINI LEO

MV. BUKOBA - DAIMA TUTAWAKUMBUKA

Chini ni mnara wa kumbukumbu ya eneo ambalo walizikwa watu waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba hiyo mnamo Mei 21.1996. Leo ni tarehe 21 mei, siku ambayo kila mwaka watanzania wanaadhimisha tukio la ajali mbaya iliyowahi kutokea katika nchini iliyohusisha kuzama kwa meli ya MV Bukoba ndani ya ziwa Victoria. Leo ni miaka 19 tangu kutokea ajali hiyo.

Wednesday, 20 May 2015

TAHADHARI KUHUSU SIMU ZA MKONONI

Ila pia..................simu hizi zina vituko.

Huku ‪#‎whatsapp‬ kuna vituko watu na status zao:
1. Mtu ameandika “‪#‎Sleeping‬” , sasa leo siku ya
tano, si kashakufa huyu?
2. Mwingine kaandika “‪#‎Driving‬” toka mwaka jana
Agosti, naona atakuwa anakaribia China
saa hizi!
3. Haya jamaa najua kalazwa anaumwa lakini
kaandika “‪#‎Happy‬” we vipi ndugu yangu?
4. Huyu mdada kaandika “‪#‎Available‬”. Sijui anajua
maana yake? Tukikuibukia utaanza mitusi!
5. Huyu nae hajabadilisha status mwaka wa pili
sasa, “‪#‎Hey‬ there! I’m using WhatsApp” sasa
unadhani sijui Tungekutanaje kama hutumii
Whatsapp?
6. Superstar wetu mmoja kaandika “‪#‎Urgent‬ calls
only”. We vipi? Kwani we Fire(fanya), au
Ambulance au polisi?
7. Haka kabishoo kameandika “‪#‎Can‬’t talk,
WhatsApp only”. Sasa una simu ya nini? Si uitupe
uwe unashinda Facebook? Simu kazi yake ya
kwanza kuongea sio
Whatsapp!
8. Huyu mshamba kaandika “‪#‎At‬ the movies” wiki
ya saba sasa, sinema gani ndefu hivyo wewe? Au
unafanya kazi ya kuuza tiketi hapo sinema?
9. Dogo kaandika “#At school” sasa Whatsapp ya
nini? Utapata Div O wewe!
10. Hahahahahaha eti “‪#‎Battery‬ about to die”
miezi sita mfululizo, badilisha hiyo betri? Au mtaa
wenu hakuna umeme miezi sita
hujachaji simu? Si kalalamikeni TANESCO? Au
nikununulie jenereta? Unaudhi!
11. Hivi najiuliza we mdada huu mwezi wa nne
sasa eti “#At the gym” unajitayarisha kwa
Olympics!
12. Bosi status yako ya “‪#‎In‬ a meeting” mwezi
mzima inachekesha, maliza huo mkutano rudi
kwenu.
WAHUSIKA BADILISHENI KABLA
SIJAWABLOCK!

Tuesday, 19 May 2015

RAIS WA MSUMBIJI BUNGENI DODOMA LEO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Anna Makinda akimkaribisha Rais wa Msumbiji
Felipe Jacinto Nyusi katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo Rais huyo alilihutubia Bunge
Rais Wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi akipokea heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi,Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi waandamizi katika serikali ya Msumbiji wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Rais wa Msumbiji kulihutubia Bunge lao mjini Dodoma(Picha na Freddy Maro)

MAENDELEO YA TERMINAL 3 YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA JULIUS NYERERE

Terminal 3 ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere unaendelea kujengwa na awamu ya kwanzan inatarajiwa kukamilika Juni 2016. Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango ndg Florance Mwanri alitembelea leo kujionea hali ilivyo na kutoa ushauri wa uboreshaji zaidi