Monday, 4 January 2016

SHULE 6 KUANZA KUFUNDISHA SOMO LA LUGHA YA KICHINA

WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imeteua shule sita za sekondari nchini kuingia katika mpango maalumu wa wanafunzi wake kufundishwa somo la lugha ya Kichina kuanzia mwaka huu.Kutokana na uamuzi huo, walimu 12 kutoka China wamekamilisha utaratibu wa mpango kazi wa namna ya ufundishaji wa somo hilo kwa shule zilizoteuliwa mara zitakapofunguliwa rasmi mwezi huu.

SERIKALI YAINUNULIA MUHIMBILI MASHINE YA CT SCAN MPYA


Naibu Waziri wa Afya , maendeleo ya jamii, jinsia , wazee na watoto Dokta Khamis Kigwangwala leo ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili -MNH- na kuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma za kulipia kwa kiwango cha daraja la kwanza ili kuongeza mapato ya hospitali na pia mgonjwa aweze kuona thamani ya pesa yake.

Akizungumza mara baada ya kutembelea hospitali hiyo ikiwemo Idara ya magonjwa ya dharura na ajali pamoja na mashine za CT Scan na MRI , Dokta Kigwangala amesema watumishi wa MNH hawanabudi kuwa wabunifu ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zina kuwa bora zaidi na zenye faida .

“ Hospitali ya Taifa Muhimbili ina madaktari bingwa wengi na wenye uwezo mkubwa wa kutoa huduma na wengine ni wataalam wa magonjwa mbalimbali ikiwemo moyo na figo hivyo naamini wanaweza kufanya mabadiliko makubwa “ amesema Kigwangala .

Awali Mkuu wa Idara ya Mionzi Dokta Florah Lwakatare amemueleza Naibu Waziri Kigwangala kwamba mashine ya mpya ya CT Scan ambayo imenunuliwa na serikali inaendelea na majaribio pamoja kuwapatia mafunzo watumishi wake kwakua kua mashine hiyo ni ya hali ya juu sana .

Amefafanua kuwa mashine hiyo ya kisasa inafanya kazi kwa haraka na kwamba tangu ianze majaribio hapo juzi mpaka leo tayari wagonjwa 26 wameshapimwa .

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Lawrence Mseru amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa MNH itaendelea kutoa huduma bora za afya

Sunday, 3 January 2016

JUMBA LA MCHUNGAJI LWAKATARE KATIKA MSUKOSUKO WA ALAMA X

Mchungaji a Kanisa la Assemblies of God,Mikocheni, Dr Getrude Lwakatare amepinga nyumba yake kubomolewa ikiwa ni siku chache baada ya wizara ya maliasili na utalii kupitia wakala wa misitu Tanzania (TFS ), kuweka alama ya X wakidai imo katika hifadhi ya bahari.

KATUNI YA LEO

Masoud Kipanya tena, anawasilisha tatizo lililopo katika wakati uliopo. Ni sahihi, si kila jambo ni la kumsubiri Magufuli. Ni wajibu wa jamii. Na mwalimu huyu naye ni sehemu ya jamii. Je, ni sababu zipi zinazompelekea aache kufundisha na kufanya biashara ya bodaboda? Kama kazi ya ualimu aliomba mwenyewe, hakulazimishwa. Na kama mshahara anapata kwa wakati. Hana sababu ya kufanya anachofanya wakati wa kazi, labda iwe jioni au kwenye likizo yake. Na hata kama ni jioni na kwenye likizo, mwalimu hapaswi kuonyesha mfano mbaya kwa kubeba abiria mishikaki!

Saturday, 2 January 2016

MAJANGILI WA WANYAMA PORI KUKIONA CHA MOTO

Mmoja wa Majenerali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania walioteuliwa kushika nyadhifa nyeti serikalini,Meja Jenerali Gaudence Milanzi,ameanza kazi kwa kutoa tahadhari kwa majangili akisema atatumia mbinu za medani kuwakabili na kuwatokomeza kabisa.

Akizungumza Muda mfupi baada ya kuapishwa mbele ya Rais John Magufuli kuwa Katibu Mkuu Wizara Ya Mali Asili na Utalii,Meja Jenerali Milanzi alisema ni aibu Tanzania kuendelea kupoteza wanyama pori bila hatua stahiki kuchukuliwa.

"Siwezi kuvumilia kuona serikali ikishindwa kusimamia rasilimali za nchi ambazo ndizo zinaoongeza idadi ya watalii nchini na pato la taifa.Majangili wanaongozwa na uchu na uchoyo kwa watanzania wengine.

"Maliasili zilizopo ni kwa ajili ya kuwanufaisha watanzania wote na kuliletea sifa taifa letu.Ni aibu kuonyesha dalili za kushindwa katika mapambano dhidi ya ujangili.Maliasili na utalii ndio kitovu cha mapato ya taifa, kwani wanyama hasa wale adimu ndio huvutia watalii.

"Nitatumia mbinu na uwezo wangu wa kijeshi kukabiliana na hilo,kwa sasa ni mapema kusema lolote.Kuna mambo mengi ninatakiwa nijifunze kwanza,lakini tutaangazia matatizo yote yanayoikabili wizara hii nyeti.

"Kuna masuala ya vitalu vya uwindaji,kuna tatizo la wananchi kuwepo ndani ya hifadhi za taifa;yote tutayaangazia pamoja na kuangalia namna ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi na ujangili." Alisema Meja Jenerali Milanzi.
Mhe.Meja Milanzi siku akila kiapo

MACHINJIO YA VINGUNGUTI YATATULIWA KERO ZAKE


Mawaziri kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mh:Kigwangallah,Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mh:Bonah,Watatu kutoka kulia ni Mh:Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mh:Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.
Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Mh:Rais John Pombe Magufuli mara baada ya tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo.

Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo,lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.

Hii leo mapema majira ya saa 3:asubuhi,Mwigulu Nchemba anarejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mh:Simbachawene(TAMISEMI) na Mh:Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.

Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.

Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tar 24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa,Vilevile wahakikishe jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.

Pili,Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa pugu,badala ya hapo makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.

Tatu,Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi(wadau) kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwaajili ya kutunzia nyama,Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa.

Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.

Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mh:Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na mkurugenzi kwaajili ya hatua Zaidi.

Simbachawene ameenda mbali Zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo.

Kwa upande wa Afya,Naibu waziri wa Afya Mh.Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg.Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo,Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na Uongozi wa machinjio utenge ofisi maalu ya kupima watu hao.

Friday, 1 January 2016

MHE RAIS MAGUFULI NA MKEWE WAMJULIA HALI MWADHAMA POLYCARP

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo January 1, 2016. Kardinali Pengo alilazwa hospitalini hapo jana jioni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

NAWATAKIA KHERI YA MWAKA MPYA 2016