Tuesday 14 October 2014

NYERERE DAY

WATANZANIA leo tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa muasisi na Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, 1999 akiwa nchini Uingereza alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu.
Maadhimisho ya siku hii kitaifa yamefanyika huko Tabora sambamba na sherehe za kuzima Mwenge mgeni rasmi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe Jakaya Mrisho Kikwete
Juu ni picha wakati wa siku za maombolezo ya kifo cha Baba wa Taifa mwaka 1999
Kiongozi wa mbio za Mwenge mwaka huu ndg Rachel Kassandra akimkabishi mhe,Rais Kikwete mwenge wakati wa kilele cha mbio hizo huko Tabora
Makamanda wa Mwenge wa Uhuru

No comments:

Post a Comment

Maoni yako