Monday 20 October 2014

EBOLA YALETA HOFU MWANZA

Watu sita wakiwamo wahudumu watatu wa afya wa hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, wamewekwa chini ya uangalizi maalum baada ya kumhudumia mgonjwa aliyefariki akiwa na dalili za ugonjwa wa ebola.Mtu aliyefariki alitajwa kuwa ni Salome Richard (17), anayetoka katika kijiji cha Kahunda wilayani Sengerema.

Akithibitisha kuwapo kwa hali hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Wilaya ya Sengerema, Dk. Mary Jose, alisema mgonjwa huyo alifikishwa katika hospitali hiyo na ndugu zake watatu akiwa na homa kali huku akitokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake.Alisema vipimo vya mgonjwa huyo vimepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Nairobi Kenya kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako