Saturday 24 December 2016

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UAGIZAJI WA NYAMA YA KUKU KUTOKA NJE YA NCHI

Serikali imepiga marufuku kuagiza na kuingiza nyama za kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi ili kulinda afya za walaji wa bidhaa hiyo ya nyama nchini.
Katazo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole Nasha kwenye mahojiano maalum na EATV ilipotaka kupata ufafanuzi wa serikali kuwa inahakikisha vipi nyama na vitoweo kutoka nje ya nchi zinaingizwa nchini zikiwa na ubora unaokidhi viwango vya afya kwa walaji.Ole Nasha amesema hairuhusiwi kuagiza wala kuuza kuku waliochinjwa kutoka nje ya nchi kwakuwa kwa sasa nchi inajitosheleza na inajitegemea kwa kiwango kikubwa cha nyama.
Amewataka wafugaji na wafanyabiashara kutumia fursa za kuzalisha nyama kwa tija na ubora zaidi ili nchi ianze kuuza vitoweo vya nyama hasa kuku nje ya nchi.
Ameongeza kuwa tayari serikali inaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa viongozi wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kuingiza nyama hizo za kuku wa nje nchini

No comments:

Post a Comment

Maoni yako