Wednesday 28 December 2016

MAAMUZI YA RUFAA YA KESI YA MHE GODBLESS LEMA KUJULIKANA JAN 4,2017

Na.Vero Ignatus Arusha.
Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa yayaliyowasilishwa na upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo upande wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya maandishi hapo kesho tarehe 30 disemba 2016
Aidha rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maamuzi ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa mshtakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa mshtakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa Lema masharti ya dhamana
Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 desemba 2016 ambapo tarehe 2 januari watakutana pande zote kwa ajili ya kufanya majumuisho na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017
Hata hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya kisheria?
Kwa upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu moja
"Unajua leo rufaa mbili zimegongana ile ya upande wa jamhuri na ile ya kwetu sisi,hivyo basi sisis tumeiomba mahakama kusitisha rufaa yetui isikilizwe ile ya serikali kwanza,kwani rufaa zote zinaelekea upandemmoja ,wandege apande ndege na wa basi apande basi "alisema Kibatala.
Hata hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless Lema amerudishwa rumande hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakama.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako