Saturday, 5 November 2016

MHE DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATIMIZA MWAKA MMOJA WA URAIS

Leo na mimi nipaze sauti yangu imfikie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa Mafanikio Makubwa aliyoyapata ktk kipindi cha Mwaka mmoja wa utawala wake tangu aingie madarakani mnano Novemba 05, 2015.

Rais Magufuli kwa kiasi kikubwa amerudisha nidhamu kwa watumishi wa umma. Leo ofisi nyingi za utumishi wa umma zina nidhamu ya hali ya juu sana, watu wanatambua vizuri nini wanapaswa kufanya na nini hawapaswi kufanya ktk Utumishi wao. Huduma zenye kukidhi matakwa ya wananchi zimerejea.

Rais Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali kwa kuzuia na kufuta matumizi yasiyokuwa ya lazima kama safari za nje ambapo ktk kila safari kwa sasa ni lazima Ikulu ibariki kwa kutoa Kibali na kuruhusu idadi ndogo tu ya watu na mara nyingine mabalozi kuiwakilisha Tanzania, kuondoa posho zisizo za lazima n.k

Rais Magufuli alielekeza fedha mbalimbali ambazo zilitengwa kwa matumizi Maalum Mfano Fedha kwa ajili ya Semina kwa Baraza la Mawaziri, Fedha kwa ajili Sherehe ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Uhuru - 09 Desemba 2015 n.k Mh. Rais alielekeza zikafanye Shughuli za Kimaendeleo ikiwemo kununua Vitanda vya Hospitali ya Taifa Muhimbili na kutengeneza Madawati kwa ajili ya Shule za msingi ili kuboresha Elimu.

Rais Magufuli alituahidi endapo atachaguliwa Elimu ya msingi na Sekondari itakuwa ni BURE ambapo ametimiza sasa Elimu kwa Shule za Msingi na Sekondari ni BURE kabisa.

Rais Magufuli aliahidi atafufua Shirika la Serikali la Ndege la ATCL kwa kununua Ndege Mpya ambapo tayari Mheshimiwa Rais ametimiza Ahadi yake kwa Kununua Ndege Mbili Mpya na leo ameahidi kutuletea Ndege Kubwa aina ya Boeing yenye uwezo wa Kubeba abiria zaidi ya 240 ili kukuza uchumi wa Nchi kupitia Sekta ya Utalii.

Rais Magufuli amefanikiwa kusimamia ipasavyo Ukusanyaji wa Mapato ya serikali na Kudhibiti Matumizi yake. Hongera pia Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais ktk hili.

Rais Magufuli alituahidi kupambana na Ufisadi na Kuendeleza Vita dhidi ya Wala Rushwa kwa Kuanzisha Mahakama ya Kushughulikia Ufisadi na Rushwa na tayari mahakama ya Kushughulikia Ufisadi & Rushwa inaishi na leo naamini imesikiliza Kesi moja.

Rais Magufuli ameendelea kuboresha barabara kwa Kukijenga kwa Kiwango cha lami mfano kama ile ya Mwenge Dar es Salaam & Mwanza.

Mheshimiwa Rais aliahidi kuhamishia Serikali yake Makao Makuu ya Tanzania Mjini Dodoma na tayari amekwisha anza kutekeleza kwa kuhamisha Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara mbalimbali.

Rais Magufuli aliahidi kukuza Uchumi wa Nchi yetu kwa kuifanya Tanzania ya Viwanda na wote tumeshuhudia Juhudi za Mheshimiwa Rais za Kutafuta wawekezaji kutoka Mataifa mbalimbali duniani ili yawekeze nchini.

Ndugu zangu yako Mengi sana aliyofanya Rais Magufuli mwenye macho haambiwi tazama ila naomba niishie hapo. Ijapokuwa Bado Changamoto ni nyingi na watu wataona Maisha yamekuwa magumu lakini tutambue na kuelewa hali hiyo haina budi kuja kwani Nchi iko katika kipindi cha Mabadiriko ya kiuchumi kitaalamu tunaita " TRANSITION PERIOD " ambapo kutokana na Juhudi za Mheshimiwa Rais kuujenga uchumi wa Nchi yetu ni lazima mwanzoni tutaona Mabadiriko fulani fulani hivyo Watanzania wenzangu tuvute subira kwa maisha Mazuri yaja. Tumpe nafasi Mh. Rais apambane kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yetu na sisi kwa nafasi zetu tumpe ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi kwa Bidii sana.

Ama Kwa Hakika Rais wetu anastahili pongezi nyingi sana na Mimi Robert PJN Kaseko Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha nichukue nafasi hii kukupongeza Rais wangu na Mwenyekiti wangu CCM Taifa Mh. DKT. John Pombe Magufuli kwa kutuletea Maendeleo makubwa na Mabadiriko ya kweli kwa kipindi cha Mwaka mmoja tunashirikiana toka tukuchague utuongoze, Mabadiriko ambayo kiukweli sisi Wananchi wa Tanzania tulisubiri kwa Muda mrefu sana na nizidi kukutia moyo Mh. Rais usirudi nyuma endelea mbele tunatambua vikwazo ni vingi na Kazi ni ngumu lakini namuomba Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu, akupe afya njema na ulinzi wake ili uendelee vyema kuwaletea Maendeleo Wananchi wako maana wewe ni Mchapa Kazi Kwelikweli tunakufahamu vizuri. HAPA KAZI TU. CCM Hoyeeeeeee.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha
November 04, 2016.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako