Friday 7 February 2014

WABUNGE WA BARAZA LA KATIBA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Florence Turuka akitangaza majina ya wabunge hao jijini Dar es salaam TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA UTANGULIZI 1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (*The Constitutional Review Act, Cap 83*). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika. 2. Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:- (i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; (ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na  (iii) Wajumbe *201* kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika. 3. Makundi hayo ni kama ifuatavyo:- (i) Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (20) (ii) Taasisi za Kidini (20) (iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42); (iv) Taasisi za Elimu (20); (v) Watu wenye Ulemavu (20); (vi) Vyama vya Wafanyakazi (19); (vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10); (viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10); (ix) Vyama vya Wakulima (20); na (x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).

No comments:

Post a Comment

Maoni yako