Friday 3 March 2017

HATIMAE MHE MBUNGE GODBLESS LEMA AACHIWA KWA DHAMANA

Hatimaye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema baada ya kusota gerezani kwa zaidi ya miezi minne. Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kupitia hoja za pande zote mbili zilizowasilishwa mahakamani hapo leo na kuamua kuzitupitilia mbali hoja za upande wa serikali za kumnyima Lema dhamana.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, Jamhuri ilikusudia mabaya kwangu lakini Mungu alikusudia mema kwetu, vilevile namshukuru sana mke wangu, kama ningepata fursa ya kuoa tena ningemuoa yeye.. Nikisema niongee ninachotaka kuongea, leo sitaweza, nimeandaa waraka kwa ajili ya mheshimiwa Rais na nitautoa huo waraka hivi karibuni katika siku ambayo tutawatangazia. Nimeona mateso mengi ya watu, mambo mengi ambayo nafasi hii haitoshi.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako