Thursday, 9 July 2009

MATUMIZI MAZURI YA KODI ZA WANANCHI

Basi la mtandao likisubiri walipa kodi waje kubofya

Madhari ya Ndani ya basi la mtandao.Kwenye ile pazia ya blue
ni kachumba kwa ajili ya kufundisha bure matumizi ya mtandao
Hili ni basi jingine nchini China


AJALI SI MAGARI,NDEGE NA MELI TU, HATA BAISKELI

Tuesday, 7 July 2009

AJALI SINZA


Ajali mbaya imetokea leo alfajiri katika maeneo ya Sinza, Kamanyola. Inasemekana kuwa ajali hiyo imetokea baada ya dereva aliyekuwa akiendesha gari lililopata ajari (Pichani) alipojaribu kulipita gari la mbele yake (Picah haikuweza kupatikana) huku kwa mbele kulikuwa na gari jingine iliyokuwa ikija kutokea Mwenge, kutokana na ufinyu wa barabara kwa mahali hapo kwani kulikuwa ni katikati ya daraja dereva wa gari iliyopata ajari hakuwa na jinsi bali kutumbukia daraji kama mnavyoona pichani.

SABASABA DAY

Leo ni Sabasaba, siku ambayo miaka iliyopita tulisherehekea sikukuu wa wakulima. Hii ni katika kukumbuka siku ya kuzaliwa TANU 7/7/1954 chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika baadae Tanzania

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA MAPOROMOKO YA VICTORIA-ZAMBIA

Mama Salma Kikwete (kushoto) akiongea jambo na Mke wa Rais wa Zambia Mama Thandiwe Rupi (kulia) wakati walipotembelea maporomoko ya Victoria yaliyopo katika mto Zambezi Nchini Zambia. Mama Kikwete ameambatana na JK katika ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini humo.

Mama ukirudi, karibu utembelee pia Maporomoko ya Sanje (Sanje waterfalls) yaliyopo Udzungwa Morogoro.

WAZIRI MKUU ATOA CHANGAMOTO JUU YA UTAMADUNI KATIKA UNENGUAJI

MANDHARI SAFI YA CHUO KIKUU KIPYA DODOMA

MALI ASILIA NA MISIMU YAKE

Nyanya na viazi vyavutia macho kweli kweli. Ni mazao asilia ya nyumbani. Hapa ni maeneo ya Msimbazi Jijini Dar.
Ni msimu wa machungwa na machenza sasa. Nyumbani ni furaha ya kupata juice asilia (Natural/fresh juice). Machungwa na machenza hulimwa kwa wingi wilayani Muheza Tanga. Tujitahidi kula matunda haya mazuri kwa afya yetu. Ushauri huu hutolewa kwa lugha ya kiingereza "A fruit a day, keeps the doctor away", ni namna nyingine ya kusema matunda hutupatia afya na kutuepusha na maradhi.

CHUO KIKUU KINGINE KIPYA KUJENGWA DAR

Na Moshi Lusonzo

umla ya shilingi bilioni 50 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu kipya Jijini Dar es Salaam ambapo ujenzi wake umeshaanza rasmi.
Chuo kikuu hicho kitakachoitwa United African, kinajengwa katika eneo la Vijibweni, Kigamboni Jijini, kwa msaada wa watu wa Korea ya Kusini, Marekani na Tanzania.

Akizungumza hivi karibuni, Msimamizi Mkuu wa ujenzi wa Chuo hicho, Mchungaji Joshua Lee, amesema chuo hicho kitakuwa na vitivo mbalimbali vya elimu pamoja na viwanda vitakavyotumika kujifunzia kivitendo.

Akasema, majengo ya chuo hicho yatajengwa ndani ya eneo la ekari 300, ikiwa ni pamoja na majengo mbalimbali ya huduma za kijamii.

Mchungaji Lee akasema kwa kuanzia, tayari miradi miwili ya jengo la ufundi stadi na ofisi mbalimbali imekamilika.

"Ujenzi utafanyika kwa awamu, hivi sasa tumeanza awamu ya kwanza kwa kujenga majengo mawili yatakayotumika kwa mafunzo ya ufundi stadi, awamu ya pili itakuwa hospitali na baadhi ya madarasa ya wanafunzi," akasema.

Akaongeza kuwa chuo hicho kitakuwa cha pekee katika ukanda wa Afrika na kwamba wanafunzi watajifunza kinadharia na vitendo chuoni hapo, pasi na matatizo.

"Tunajua wapo Watanzania wenye upeo mkubwa sana. Lakini wameshindwa kuonyesha vipaji vyao kutokana na kukosa nyenzo... tutawapa fursa ili wawe na uwezo zaidi pindi watakapomaliza kwenye chuo hiki," akaongeza.