Wednesday, 5 August 2015

Monday, 3 August 2015

CCM: DKT MAGUFULI KUCHUKUA FOMU YA URAIS NEC KESHO

MGOMBEA mteule wa urais kwa tiketi ya CCM,
Dk. John Magufuli, kesho Jumanne, Agosti 3, 2015, atatinga Tume ya Taifa
ya Uchaguzi, kuchukua fomu ya kuomba kugombea Urais katika uchaguzi
mkuu utakaofanyika Oktoba Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa
habari, leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape
Nnauye amesema, Msafara wa Dk. Magufuli kwenda kuchukua fomu hiyo,
utaanza saa tano asubuhi ukitokea Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM,
Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam.

Nape amesema, msafara ambao
utaambatana na shamrashamra za aina yake, utapita katika Barabara za
Morogoro, Bibi Titi Mohammed na Ohio kabla ya kufika Ofisi za Tume ya
Taifa ya Uchaguzi zilizopo Posta House, karibu na makao Makuu ya Jeshi
la Polisi.

Amesema, Dk. Magufuli ambaye ataambatana na Mgombea
mwenza wake, Samia Suluhu Hassan, mbali na makada, wapenzi na wanachama wa CCM,
atasindikizwa na viongozi mbaimbali wakiwemo, Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Bara) Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Dk.Magufuli alichaguliwa na Mkutnao Mku wa CCM, uliofanyika Oktoba 11,
2015, mjini Dodoma, baada ya kuwashinda wagombea wenzake, Dk. Asha-Rose
Migiro na Amina Salum Ally

KURA ZA MAONI ZATIKISA VIGOGO WA CCM

MANCHESTER UNITED FC YATAMBULISHA JEZI ZAKE MPYA 2015/2016

Baada ya miaka 13 ya matumizi ya jezi za Nike, Manchester United sasa imeamua kuzindua jezi mpya zitakazotumika katika msimu wa 2015/2016. Man United watatumia jezi zitakazokuwa zinatengenezwa na Kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas ya nchini Ujerumani

AZAM FC YATWAA UBINGWA KOMBE LA CECAFA. WAIPIGA GOR MAHIA YA KENYA 2-0

Timu ya AZAM FC ya jijini Dar imetwaa kombe la CECAFA maarufu kama Kagame Cup kwa kuichapa Gor Mahia ya Kenya kwa mabao 2-0. Walikabidhiwa kombe hilo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Meck Sadiki akishirikiana na Waziri wa Zamani wa huko Kenya mhe. Raila Odinga. Pia walikabidhiwa kitita cha dola elfu 30. (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

DR.MAGUFULI ALIKOTOKA NI MBALI

Alizaliwa mwaka October 29 1959 kwahiyo umri wake ni miaka 55 akiwa na headlines nyingi za uongozi alioanza nao mwaka 1995 alipokuwa pia naibu waziri wa kazi na leo hii ndiye mgombea Urais wa Tanzania 2015 kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.

Hii picha yake hapa chini ni ya miaka 40 iliyopita akiwa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Katoke Seminari March 1975, sura imepotea au yuleyule?
Hapa chini ni Dkt.John Magufuli alipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika muhula wa masomo wa 1985/1986. Wengine katika picha kushoto ni Dkt. Abel Minani na kulia ni Dkt. John Kyaruzi

Sunday, 2 August 2015

NYERERE ALIVOMZUNGUMZIA MHE.EDWARD LOWASSA


Hotuba ya Mwalimu Nyerere huko Mbeya 1995 kuhusu kukimbilia IKULU

ASEMAVYO DR.SLAA

Sijatoweka, sijajificha, sina sababu ya kufanya hayo katika nchi huru. Niko salama na buheri wa afya. Niko katika tafakari, nitazungumza

Saturday, 1 August 2015

MWAMBIE MUNGU ASANTE KWA ALIVYO KUUMBA

BASATA LAMPA ADHABU MWANAMUZIKI SHILOLE

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limemfungia mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole” kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na kukiuka sheria na maadili.

Barua ya BASATA imesomeka hivi “Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili”.

“BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako”.

"Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae”.
Shilole katika Onyesho nchini Ubelgiji