Sunday 25 January 2015

MABADILIKO: UTEUZI WA MAWAZIRI NA MANAIBU

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amebadili mawazini na naibu mawaziri Ikulu jana.
Akitangaza mabadiliko ya mawaziri hao jana, Katibu Mkuu Kiongozi wa Ofisi ya Rais, Sifue Ombeni alitaja mawaziri hao wapya ambao wanaapishwa jana jioni hii na wizara zao kwenye mabano kuwa George Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk. Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).
Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira (Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama (Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji).
Rais pia ameteua manaibu waziri na wizara zao kwenye mabano kama ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati na Madini).

No comments:

Post a Comment

Maoni yako